KUMBILAMOTO AANGUSHA NG'OMBE KUWASHUKURU WAPIGAKURA , NA KUWAAHIDI VINGUNGUTI MPYA.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Diwani wa Vingunguti
Omary Said Kumbilamoto
amewashukuru wananchi na wapigakura wa kata hiyo kwa kumchagua tena kuwa Diwani
wa kata hiyo baada ya kujiunga na Chama
Cha Mapinduzi CCM akitokea Chama cha wananchi CUF .
Kumbilamoto ametoa shukrani hizoleo katika makao makuu ya
CCM kata ya Vingunguti alipo kuwa
amweaandalia sherehe ya shukrani wananchi waliomuungamkono na kusema kuwa sasa
kilicho baki ni kuwatumikia wananchi hao na kwamba hanachakuwalipa ila shukrani
.
Aidha amesema
baadaya uchaguzi kumalizika sasa nikufanyakazi kutimiza ahadi alizo
waahidi wananchi wa katahiyo ikiwemo kutatua kero za babara,Afya maji ,Elimu na
Maji ambazo ndizo zinzonekana kuwa changamoto katika eneo hilo.
‘’Nashukuru kazi ya ujenzi wa barabara ya
kwamnyamani inakaribia kumalizika nilipamabanasana ili ijengwe ujenzi
wamachinjio ya kisasa ya vingunguti nayo karibuni ujenzi unaanza pamoja na barabara ya barakuda na mchakato wa kuomba pesa kwa
TARURAukokaribu kukamilika ,lakini pia wataalamu wanafanya tathimini ya kuonagharama
kiasi gani ya umeme utatumika ili tuweze kuwa taaza barabara zetu za mtaa’’
alisema.
Kwaupande wake Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara ambaye naye
alichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika
tarehe 16 septemba amempongeza Diwani
Kumbilamoto kwa kuchaguliwa na kwakuwajali wananchi wake kwa kulanao chakula na
kuwashukuru na kuahidi kutoa ushirikianao
ilikuweza kuwaletea wananchi wa
vinguti na Ilala kwa pamoja.
‘’ Tumechaguliwa na wananchi ili tuwatumikie ndugu
wananchi wa Vingunguti nawahidi katika kuleta maendeleo ya Manispaa yetu ya Ilala mimi na diwani wenu
tutashirikiana katika mambo ya maendeleo najua bado mnazochangamoto nyingi kama
sisi huko Ukonga lakini tutazitatua mojamoja hadi ziishe’’ alisema.
Nao baadi ya wananchi wakatahiyo walifika tika sherehe
hiyo wamesema wamekuwa na madiwani wengi
waliopita katika katahiyo lakini
Kumbilamoto ni mtu mwenye moyo watofauti na nimmtu anaye jail waytu wake
anashiriki katika matatizo yao na hata katika mazuri pia amekuwani mtu ambaye
yuko kutumika ,kutoaushauri na msaada kwa muda wote.
‘’Ametuchinjia Ng’ombe tumekula naye tumejipongeza kwa
ushindi na amaetuambia kuwa sasa ni
mwanzo mpya mwingine wa kutuwakilisha , sisitunaahiditu kumpaushirkiano na tunaimani naye, hatawewe ndugu mwandishi kama ulivyo uona
umati huu niishara ya kuwa Diwani wetu anakubalika na watu wa vyama vyote hawawengine wilikua humu ni wapinzani lakini
kwa Kumbilamoto ni wote ni wamoja” alisema
Badhi ya Majungu ya chakula na mahanjumati ya chakula kilicho anadaliwa na Diwani Kumbilamoto kujipongeza na wapigakurawake baadaya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi uliofanyika tarehe 16 / Sept/20189 (Picha zote na Mwamba wa habari)Wananchi wakigawiwa chakula katika sherehe ya shukrani iliyo andaliwa na Diwani wa Vingungti Omary Kumbilamoto .
Diwani wa Vingunguti Omary Kumbilamoto akitoa neno la shukrani kwa wananchi walio jumuika naye katika sherehe ambayo aliwaandaalia.
Munge wa Ukonga Mwita Waitara akiwasalimu wananchi wa katikasherehe na kuwa shukuru kwa kumchagua Omary Kumbilamoto na CCM kwa ujumla.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma akizungumza na wananchi wa Vingunguti aliye upande wa kulia hap chini ni Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara naye alifika kuungamkono Diwani Kumbilamoto.






Post a Comment