Jamii yashauriwa kuyatunza na kuhifadhi mazingira kuepuka magonjwa
Hussein Ndubikile,
Mwambawahabari
Ikiwa imebaki siku moja dunia kuadhimisha Siku ya Afya ya
Mazingira jamii imeshauriwa kuyatunza na
kuyahifadhi mazingira ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko yatokanayo
kushindwa kuviweka vyakula katika mazingira ya usafi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Usafi ya ya Kajenjere Trading Company ltd, Mathew Amwali
wakati wa shughuli ya ufanyaji usafi katika Soko la Buguruni uliofanywa na
Kampuni hiyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara, viongozi wa soko na wadau wa
usafi.
Amesema kutokana na jamii kutozingatia kanuni na sheria za
usafi wa mazingira huchangia kutokea magonjwa ambukizi yakiwemo ya Kipindupindu,
kuhara huku akibainisha takataka zinaweza kutumika njia ya kujipatia kipato.
“Takataka ni fursa ya kujipatia kipato mtu akiweza
kuzitenganisha sio kuzichanganya mfano chuma, karatasi na maboksi
taka zitokanazo na mahindi, mbogamboga
zinaweza kuzalisha molea ya samadi, “ amesema.
Amebainisha kuwa kampuni yake inaunga mkono kauli ya Mkuu wa
mkoa huo, Paul Makonda ya kuhakikisha jiji linakuwa katika hali ya usafi na
kwamba wako tayari kuzoa taka usiku ili kuondokana na adha ya msongamano muda
wa asubuhi na mchana.
Amesisitiza kuwa kauli mbiu ya maadhimnisho hayo ni Usalama
wa Chakula kwa afya ya Jamii na uchumi wa viwanda kwa taifa na kueleza kuwa
elimu inatakiwa kutolewa kupunguza uchafu wa mazingira.
Kwa upande wake Ofisa Afya wa Mazingira wa Soko hilo,
Patrick Mazengo amesema hali ya usafi sokoni hapo imeimarika tofauti na awali
ilivyokuwa hivyo wataendelea kuhamasisha usafi wa mazingira kwa
wafanyabiashara.
Kwa upande wake Ofisa Afya wa Manispaa ya Ilala, Fatuma
Maduhu amesema manispaa hiyo itahakikisha wananchi wake wananshiriki kikamilifu
katika shughuli za ufanayaji usafi wa mazingira ili kujiepusha na magonnjwa.
Mfanyabiashara wa Soko hilo, Rashid Kawangwa amefafanua kuwa
wamehamasika kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya soko hilo na
kwamba ni endelevu.

Post a Comment