Christopher Chiza aapishwa bungeni
Mkutano wa kumi na mbili wa 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umeanza rasmi leo tarehe 4 
Septemba, 2018 ambapo ilikuwa kikao cha kwanza na kuongozwa na Spika Job
 Ndugai.
Katika kikao hicho, Mbunge wa 
Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza aliyechaguliwa kwenye 
uchaguzi mdogo wa tarehe 12 Agosti, 2018 alikula kiapo cha uaminifu 
mbele ya bunge.
Akiapa mbele ya Bunge, Mhandisi Chiza aliapa kuitumikia, kuilinda na kuitetea katiba ya nchi kwa moyo wake wote. 
Mhandisi Chiza alishinda katika 
uchaguzi mdogo uliofanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo 
kupitia Chadema, marehemu Kasuku Bilago kufariki dunia. Katika uchaguzi 
huo alichuana vikali na mgombea wa Chadema, Elia Michael.  
Post a Comment