Ads

NHIF YAPATA CHETI CHA KIMATAIFA UTOAJI HUDUMA BORA.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam
MMG_5853
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akikabidhi Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda kilichotolewa na Taasisi ya BSI (British Standards Institute) kwa Mfuko huo leo Agosti 20, 2018.
MMG_5864
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda (katikati) naye alikabidhi cheti hicho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
MMG_5879
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akionyesha cheti hicho kwa wageni mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo.
MMG_5778
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya kupokea Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kilichotolewa na Taasisi ya BSI (British Standards Institute)  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), leo Agosti 20, 2018.
MMG_5758
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda akifurahi jambo wakati akizungumza katika hafla hiyo.
MMG_5692
MMG_5651
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa  ISO 9001:2015.
MMG_5615
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Anjela Mziray akitoa muongozo katika hafla hiyo.
MMG_5623

MMG_5624
Picha mbalimbali zikionyesha watumishi wa NHIF pamoja na wadau wakiwa katika hafla  iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
MMG_5658
MMG_5626

MMG_5630

MMG_5642

MMG_5644

MMG_5661

MMG_5663

MMG_5665

MMG_5668

MMG_5670

MMG_5677

MMG_5706
Wafanyakazi wa NHIF wakiimba nyimbo katika hafla ya kupata cheti cha ISO.
MMG_5729

MMG_5721

MMG_5678

MMG_5963

MMG_5969

MMG_5979

MMG_5993

MMG_6008

MMG_6014

MMG_6018
Serikali ipo katika utekelezaji wa kuhakikisha kila mtanzania anajiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao utamwezesha mwanachama kupata matibabu kipindi ambacho atakuwa mgonjwa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea cheti cha kutoa huduma bora Kimataifa (ISO) kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa serikali itahakikisha watanzania wanakuwa bima ya afya.

Ndugulile amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakikosa fedha za matibabu na kushindwa kumudu gharama.

Amefafanua kuwa lengo la serikali ni kufikia asilimia 50 ya watanzania ambao ni wanachama wa NHIF, kwani kwa sasa wapo asilimia 30.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kufikia malengo hayo NHIF inatakiwa kufungua wigo kwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya.

Katika hatua nyengine ameipongeza NHIF kwa kupata cheti cha ISO kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa viwango vya ubora kimataifa. 

"NHIF ni taasisi ambayo imekuwa ikifanya maboresho kila wakati jambo ambalo kwa sasa limeleta mafanikio makubwa" amesema Dkt. Ndugulile.

Katika kuboresha utendaji Dkt. Ndugulile amewataka watendaji  NHIF kutokaa ofisini muda wote, badala yake kuwafata wananchi katika vituo vya afya kwa ajili ya kuhamasisha wajiunge na mfuko wa bima ya afya taifa.

"Tunapaswa kuongeza vifurushi vya huduma za NHIF ili kuwapa fursa vijana ambao wapo mtaani hawana kazi na wanapenda kwa wanachama ili wapate huduma ya Afya" amesema Dkt. Ndugulile.

Amesema kuwa sekta ya Afya imebadilika sana, hivyo NHIF inatakiwa kutoa huduma za afya  kulingana na maitaji kwa sasa.

"Cheti hicho ni hatua kubwa, ambacho kimepatikana kupitia misingi ya utoaji bora za huduma ya Afya" amesema Dkt. Ndugulile.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda, amesema kuwa jambo la muhimu ni kuhakikisha shirika kuwa na sifa za kimataifa.

Amesema kuwa suala la kuwa na  viwango bora vya huduma tumefanikiwa kulipa kipaombele ili hukakikisha tunafikia malengo.

"Ifike mahali tunatakiwa kuwa na mfuko ambao utakuwa unatoa huduma bora kwa viwango vya kimataifa" amesema Makinda.

Amesema kuwa kupitia cheti hicho watahakikisha wanaendelea kutoa huduma bora katika vituo vyote vya bima ya Afya.

"Tunategemea kila mtanzania atapata huduma bora za Afya pamoja na kutengeneza mazingira rafiki ya kujiunga mfuko wetu" amesema Anne.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga, amesema kuwa kupata cheti hicho kimetoka na uimara wa utendaji wao.

Amesema kuwa wataendelea kuboresha utendaji wao kwa kuongeza ufanisi ili kuhakisha mipango ya utendaji kazi inafikia malengo.

"Watoa huduma wanatakiwa kuwa waminifu jambo ambalo litasaidia kupiga hatua katika kufikia malengo yetu" amesema Konga.

No comments