Ads

RORATY CLUB OFA AMES KUSHIRIKIANA NA SAME KULETA MAENDELEO.


 Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Mhe.Rosemary Senyamule akizungumza ofisini kwake na wadau wa Rotary Club.
 DC wa Same Mhe.Rosemary Senyamule( kulia mwenye koti jekundu) wakijadili jambo kwenye ramani.
 Rotary Club of Ames,Iowa US kwa ushirika wenza na Rotary Club of Same na Rotary International wakiwa wamejumuika kwenye mkutano wa pamoja kujadili maendeleo ya SAME

Rotary Club of Ames,Iowa US kwa ushirika wenza na Rotary Club of Same na Rotary International imeweka  alama kubwa Wilayani Same kwa kujenga miundombinu ya maji na kupunguza adha ya maji katika wilaya hiyo.

Katika ziara ya wanachama wa Rotary kutoka Same Giliard Eneza Mkubwa-Meneja wa miradi na Amon Noel Mchomvu ambaye ni Rais wa Rotary Club of Same ambao walikwenda mji wa Ames ,Iowa Marekani waliweza kuwasilisha maandiko toka sekta ya maji na ardhi.

Marafiki hao wa Rotary walikubali kuendelea kushirikiana kwa karibu na Wilaya ya Same kuhakikisha miradi hiyo inakamilika.

Aidha wameweza kutembelea jingo na ukumbi wa vikao vya Bunge na Senate ya Iowa (Iowa State Capital) na kuahidiawa kuwa mji rafiki na Wilaya ya Same ambapo eneo kubwa ya jingo hilo limepambwa kwa dhahabu inch 6.

Akiwakabidhi bendera ya Tanzania kabla ya kuondoka  Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Mhe.Rosemary Senyamule aliwataka kuonyesha maadili mema kama watanzania,chochote watakachokifanya kinawakilisha wananchi wote.

Aliwakabidhi vyeti vya shukrani kuwapelekea wadau hao wa maendeleo kama ishara ya kuthamini kile wanachokifanya kwa wananchi wa Same na Tanzania kwa ujumla.

Wakitoa taarifa ya safari ya kwa DC wa Same ,wawakilishi hao walieleza kufurahishwa mno na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya u

No comments