MJEMA ATEMBELEA BANDA NA SHAMBADARASA LA ILALA NANE NANE MOROGORO ATOA AGIZO HILI.
Na. John Luhende
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi na vijana wa Manispaa ya Ilala kujishughulisha na shughuli ndogondogo za kilimo ili kujikwamua kiuchumi na kuacha kukaa vijiweni bila kuwa na shughuli za kufanya.
DC Mjema Ameyasema hayo leo mjini Morogoro alipokuwa alipotembelea banda na shamba darasa la Manispaa hiyo katika viwanja vya nanenane na kusema kuwa biashara siyo kung'ania tu kuuza bidhaa au umachinga bali waingie pia kwa upande wa Kilimo.Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wananchi na vijana wa Manispaa ya Ilala kujishughulisha na shughuli ndogondogo za kilimo ili kujikwamua kiuchumi na kuacha kukaa vijiweni bila kuwa na shughuli za kufanya.
"Manispaa ya Ilala maeneo bado tunayo nawaomba tu Vijana wajifunze katika vikundi waje tuwape maeneo tuko tayari kuwasaidia ili waweze na kazi za kufanya" alisema.
Aidha amewataka taalamu na washiriki wa maonesho hayo baada ya muda wa maonesho kuisha kuendana katika kata kutoa elimu ya kilimo kuwa fundisha wananchi ili waweze kuwa na vipando vya katika maeneo yao.
"Tumeona wanayo tengeneza mkaa mbadala kwa kutumia taka, mbolea kwa kutumia matunda yaliyooza na mabaki ya mazoez na jinsi ya kubadili maji taka kuwa safi na kufaa kwa kilimo" alisema na kuongeza.
Post a Comment