MGOMBEA WA CUF NAFASI YA NAIBUMEYA MANISPAA YA KIGAMBONI AJITOA DAKIKA ZA MWISHO , CCM YAPETA.
Katibu
tawala wa Manispaa ya Kigamboni Rahel Mhando akitangaza matokeo ya uchaguzi wa naibu Meya wa Halmashauri, kulia ni Meya wa manispaa ya kigamboni Maabadi Hoja katikati ni kaimu Mkurugengenzi wa kigamboni David
sukali.
Diwani wa viti maalumu Zuhura Dolla CCM akipiga kura ya katika uchaguzi wa naibu
meya wa Manispaa ya Kigamboni .
Mwamba wa habari
Na John Luhende
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na mshindi wa kishindo katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Halmshauri
ya Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam ambapo mgombea wake
Diwani wa Kata ya Kibada, Amin
Mzuri Sambo , amepata kura nane kati ya
tisa zilizopigwa.
Katika
uchaguzi huo, uliofanyika leo jioni jijini Dar es Salaam, Mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye ni Diwani wa Kata ya Tungi, Ernest
Mafimbo alijitoa katika dakika za mwisho na kushangaza wajumbe kutokana na kile alichokidai hakuwa na taarifa kwamba anagombea.
“Mimi sikuwa
na taarifa kwamba nagombea, chama cha wananchi (CUF) hakijanipa barua ya kuteuliwa kushiriki uchaguzi”amesema Mafimbo, hali iliyozua hali ya sitofahamu ukumbini.
Hata hivyo
Ofisa wa Uchaguzi huo Magdalena Malunda
aliwathibitishia wajumbe kuwa, Halmshauri iliviandikia vyama vyote vyenye
madiwani katika baraza hilo na kwamba CUF ilimtambulisha Mafimbo kwa barua kuwa
ndiye mgombea hivyo inashangaa kusikia akisema hana taarifa.
Kufuatia
hali hiyo Mafimbo alitangaza kujitoa
katika kinyang’anyiro hicho hivyo
kumpa upenyo Mzurisambo kuwa mgombea pekee.
Akitangaza
matokeo mara baada ya upigaji kura kukamilika, Katibu Tawala wa Hal,shauri ya
Manispaa ya Kigamboni, Rachael Mhando alisema,
kura zilizopigwa zilikuwa tisa ambapo kura moja ilikuwa ni ya hapana hivyo kumtangaza Mzurisambo kuwa Naibu Meya.
Mzurisambo
ambaye alikuwa akitetea kiti hicho
ambacho amekiongoza tangu mwaka
2016, aliwashukuru wajumbe kwa kumuamini
na kumpa dhamana ya kuongoza tena na kwamba atashirikiana kwa karibu na
viongozi na wananchi wa Kigamboni katika kuieletea maendeleo wilaya hiyo.
Mbali na
uchaguzi huo wa Naibu Meya ambao
hufanyika kila mwaka, pia baraza
hilo lilifanya uchaguzi wa wenye viti wa kamato mbalimbali.
Post a Comment