Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Mkuranga awafuta wadaiwa wawili kesi ya AG Kilangi .
Na Hussein
Ndubikile,
Mwambawahabari, Pwani
Mwenyekiti
wa Ba Baraza la Ardhi na Nyumba la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa
wa Pwani, Rehema Mwakibuja amewaondoa
wadaiwa wawili akiwemo Omari Issa na Bakari Saguti katika kesi ya msingi msingi
ya mgogoro wa ardhi kati ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali(AG), Adelardus Kilangi ambaye ni mdai dhidi ya wadaiwa zaidi
ya 70 ambao ni wananchi wa Kijiji cha Vicheji kilichopo wilayani humo licha ya
wadaiwa hao kudai hawawezi kutoa maelezo sababu kuwa Wakili wao hayupo.
Hatua hiyo
imekuja baada ya wadaiwa hao kutakaa
kutoa maelezo kwa kuwa wakili wao alipata ajali na taarifa walishatoa huku
kila mmoja akisisitiza tayari wameshafanya mazungumzo ya awall na wakili mpya
hivyo tararibu zitakapokamilika wataaendelea na kesi.
Mwenyekiti wa baraza hilo alituipilia mbali ombi hilo
kwa kueleza kuwa kesi imeshaletwa mezani hivyo lazima iendelele kusikilizwa na
kwamba waliokataa kuzungumza amewafuta majina yao.
Kwa upande
wa mdaiwa, Juma mauge alipotakiwa kutoa maelezo alidai hawezi kuongea kwa
ufasaha kwa ametoka kwenye msiba wa mama yake mzazi, hivyo mwenyekiti
alimkubalia na kumtaka aende akajiandae atapokuja kesi iendelee kusikilizwa.
Katika hatua
nyingine mwenyekiti huyo aliwaambia wadaiwa waliofika katika baraza hilo hakuna
sheria inayoelezea wadaiwa kutoa maelezo kwa mtiririko wa watu waliowapanga hivyo
baraza hilo lina uwezo wa kumchagua yeyote kati
yao na si vinginevyo.
Mgogoro
katika kesi namba 55 ya mwaka 2016 unawahusisha wadaiwa Said Kaisi 46, Bakari
Saguti 60, Omary Issa 42, Juma Omary 40, Salima Bilali (53), Regia Issaya(55)
,Sada Abdallah(72) na ambao kwa pamoja
wanadaiwa kuingia kwenye shamba la Kilangi bila kibali.
Washitakiwa
hao kwa pamoja inadaiwa kuwa Mei 9 2016 katika Kijiji cha Vicheji waliharibu
Miti 13 ya Minazi na nyumba mbili vyenye thamani ya Sh. Mil 22.2 mali ya
AG Kilangi.
Kesi hiyo imeahirishwa
hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Post a Comment