ALICHOKISEMA MBUNGE WA CUF, KUCHAUKA BAADA YA KUHAMIA CCM
Mbunge wa jimbo la Liwale Mkoani Lindi kupitia chama cha wananchi Cuf Ndugu. Zuberi Kuchauka amerejea CCM ambapo aliondoka kwa muda mrefu tangu mwaka 2005 na kusema kuwa kurejea kwake kumetokana na Rais Magufuli kuirudisha misingi ya waasisi ambao ni TANU na ASP ambayo ilikosekana kwa muda mrefu ndani ya chama hicho.
Ameeleza kuwa sababu
za kuondoka CUF ni kuwepo kwa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu ndani ya chama
hicho na kusababisha yeye kama kiongozi kushindwa kufanya kazi ya kuwaletea
wananchi wake maendeleo na kushughulika na mgogoro kwa muda wote.
Ameendelea kusema kuwa
mkanganyiko uliopo ndani ya CUF umesababisha kuwa na makundi mawili ndani ya
chama ambayo ni CUF ya Lipumba ambaye ni Mwenyekiti na CUF ya Maalim Seif Katibu Mkuu wa chama hicho, na ukiwa katika
kundi moja wapo kati ya hayo basi unaonekana msaliti kwa kundi lingine na ndio
maana nimeamua kurejea CCM ili kuweza kuwatumikia wananchi.
Aliongezea kuwa toka Serikali
ya Awamu ya Tano imeingia madarakani katika jimbo lake wamepata zaidi ya bilioni
moja kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati mbili lakini pia serikali imepeleka zaidi ya watumishi 80 ili kuboresha huduma
jimboni humo.
Post a Comment