Ads

VIONGOZI SIMBA WATANGULIA UTURUKI.


Baadhi ya viongozi wa Simba wakiwa wanasukuma mizigo tayari kwa safari ya kwenda nchini Uturuki.
MWAMBA WA HABARI.
Baadhi ya viongozi wa Mabigwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba Sport Klabu wameanza safari ya kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na ligi Kuu inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi ujao.

Simba inakwenda kuweka Kambi Uturuki kujiandaa na msimu ujao kwa ajili ya kuhakikisha inatetea kombe la ligi.

Safari ya viongozi hao wameondoka likiongozwa na Kocha Msaidizi, Masoud Djuma pamoja na Kocha wa Makipa, Mohamed Mwarami, Daktari wa timu, Yassin Gembe na meneja wa timu hiyo.

Kundi  linakalofuatia ni wachezaji ambalo linatarajia kufunga safari ya Uturuki tayari kwa kuanza kambi hiyo.

No comments