UONGOZI WA SIMBA WATOA BARAKA KWA NDEMLA
Uongozi wa Simba umetoa baraka zote kwa kiungo wake kinda, Said Ndemla kwenda kufanya kazi nchini Sweden.
Ndemla amebaki nchini wakati kikosi cha Simba kimekwea pipa kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya.
Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema wametoa baraka zote kwa Ndemla kwenda nchini Sweden katika klabu ya AFC.
“Ndemla tumemruhusu kwenda Sweden ndiyo maana alibaki nchini. Yuko katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya safari yake ya Sweden.
“Akishafika huko sisi tutaendelea na mazungumzo na klabu yake. Lakini Simba tunapoona kuna jambo linawezekana basi ni vizuri kuwapa nafasi vijana kujiendeleza,” alisema Try Again.
AFC ni kati ya timu zinazosifika kutoa vipaji na mchezaji wa kwanza Mtanzania kuichezea alikuwa ni Thomas Ulimwengu.
Ulimwengu aliichezea AFC ambayo baadaye ilimuuza kwenye klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo. Baadaye aliondoka na kurejea katika klabu hiyo lakini alishindwa kufanya vizuri kutokana na kuwa majeruhi
Post a Comment