SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia malighafi
inayotumika kutengeneza batiki wakati alipokitembelea kikundi cha wanawake
wajasiriamali cha Jikomboe kilichopo Wilaya
ya Chato wakati akihitimishaziara yake
alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia
utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya siku
mbiliua Naibu Waziri huyo mkoani humo.
Mbunge wa Chato (CCM) na Waziri wa Madini
Mhe. Dkt. Medard Kalemani akimshukuru
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile kwa ziara yake alioyoifanya katika kata zawilaya ya Chato
mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya
jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya Naibu Waziri huyo ya siku mbili mkoani
humo.
Mwekahazina wa kikundi cha Jikomboe kilichopo
wilayani Chato Mkoani Geita akiwasilisha risala yao kwa Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wkati
wa kuhitimishwa kwa ziara yake
alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia
utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya
Naibu Waziri huyo ya siku mbili mkoani humo.
Baadhi ya wananwake wajasiriamali
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akihitimisha ziara yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya
Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo
ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri huyo mkoani
humo.
.........................................................................
Na WAMJW CHATO - GEITA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuwa hakutakuwa na riba katika
mikopo itakayotolewa kwa wanawake, vijana na walemavu katika ngazi ya
Halmashauri.
Kauli hiyo imetolewa wilayani Chato na Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndugulile alipokitembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Jikomboe.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali
imedhamiria kuwasaidia Wanawake, vijana na walemavu kujikwamua kiuchumi hivyo
imeona ni bora mikopo itolewe bila riba ili kuwapa fursa wanawake, vijana na
walemavu kwa ajili ya kuanzisha miradi ya wingi ya kujikwamua kiuchumi.
Ameongeza kuwa suala la riba limekuwa kikwazo
kwa makundi mengi kuweza kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati.
"Niseme tu tumeliangalia suala hili kwa
karibu ili tuwawezeshe wananchi hasa wanawake, vijana na walemavu kujikwamua
kiuchumi" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Akisoma risala kwa niaba ya kikundi cha Jikomboe
Mweka hazina wa kikundi hicho Bi. Deborah Jeremia amesema kuwa walifanikiwa kupata mikopo wa
Shilingi Millioni moja na kurejesha mikopo yote kwa wakati.
Kwa upande wake Mbunge wa Chato(CCM) na Waziri
wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema
kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato inashirikiana na Ofisi ya Mbunge katika
kuwawezesha wanawake, vijana na walemavu kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali
kutoka Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
"Tumewapatia mafunzo wanawake wajasiriamali
kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi" alisisitiza Dkt.Kalemani.
Post a Comment