HIZI NDIYO KLABU ZILIZOCHANGIA MAGOLI MENGI KOMBE LA DUNIA

Mfungaji aliyeongoza
kufunga magoli mengi kwenye kombe la dunia Harry Kane akiwa anatokea
katika klabu ya Tottenham Hortspur na timu ya England.
Klabu ya PSG ya Ufaransa naTottenham
Hortspur ya nchini Uingereza zimeongoza katika listi ya vilabu
vilivyochangia mabao mengi katika michuano ya kombe la Dunia
iliyomalizika hivi karibuni nchini Urusi.
PSG imeongoza ikiwa imechangia jumla ya
magoli 12, magoli manne kati ya hayo yakifungwa na Kylian Mbappe na
mengine yakifungwa na Edinson Cavani (3), Neymar (2), Thomas Meunier,
Angel Di Maria na Thiago Silva.
Spurs nayo imelingana na PSG kwa kutoa
wachezaji waliofunga jumla ya magoli 12 katika michuano hiyo huku
mchezaji, Harry Kane akifunga magoli 6 peke yake na mengine yakifungwa
na, Heung Min Son (2), Christian Eriksen (1), Dele Alli (1), Kieran
Trippier (1) na Jan Vertonghen.
Klabu ya Barcelona imechangia magoli 11
na wafungaji wakiwa ni Yerry Mina (3), Phillipe Coutinho (2), Luis
Suarez (2), Lionel Messi (1), Samuel Umtiti, Ivan Rakitic na Paulinho
ambaye amejiunga na klabu ya Ghuangzhou Evergrande kwa mkopo baada ya
kombe la Dunia kumalizika .
Real Madrid imekamata nafasi ya tatu
ikiwa imetoa wachezaji ambao wamefunga jumla ya magoli 10 kwenye
michuano hiyo, wafungaji ni Cristiano Ronaldo ambaye amejiunga na
Juventus wiki chache zilizopita akifunga magoli manne, Luka Modric (2),
Nacho, Isco, Raphael Varane na Toni Kroos.
Klabu zingine zilizochangia magoli mengi
ni Atletico Madrid na Manchezter United zilizochangia magoli 8, Villa
Real na Manchezter City zikichangia magoli 5, Liverpool, Chelsea,
Juventus na CSKA Moscow zikichangia magoli manne.
Post a Comment