Ads

WANANCHI ILALA WAIOMBA SERIKALI KUTATUA KERO YA MIUNDO MBINU

Mwambawahabari
Wanchi wa kata ya Ilala tawi la msimbazi mivinjeni wameiomba serekali kuwasaidia kutatua kero za miundombinu zinazowakabili  ikiwemo ujenzi wa barabara na mifereji ya kupitisha maji ili waweza kuwafikisha wagonjwa  hospitalini.

Hayo yamejiri kwenye mwendelezo wa ziara ya chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Ilala ya kutembea kata na mashina yake ambapo Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ubaya Chuma amesemakuwa kero hizo watahakikisha zinatatuliwa na viongozi wa maeneo hayo akiwemo mbunge na diwani wake.

Aidha wananchi hao wameiomba serekali pia kuwasaidia kupata ufumbuzi wa upatikanaji wa mikopo haswa kwa kinamama na vijana ili waweza kuendeleza biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande mwingine wakazi wa tawi la shauri moyo wamekiomba chama Cha mapinduzi kuwasaidia kutatua kero wanayokumbana nayo ya kujaa mtope katika soko la ilala na maadhi ya mifereji katika eneo hilo kujaa maji.

Akizungumza katika tawi hilo Katibu Muenezi CCM wilaya ya Ilala Said Side amewataka wakazi hao kuwa wavumilivu kwani Manispaa la Ilala imeandaa mchakato wa kuboresha masoko yote yaliyopo ndani ya wilaya hiyo.

" Tayari soko ya kisutu liko kwenye marekebisho na jitihada za seriali zipo za kutosha kwani tumeongea na Diwani wa eneo hili na fedha za kurekebisha masoko mengine tayari zishatengwa" amesema side.

No comments