Ads

SERIKALI YATENGA BILIONI 16 UJENZI SOKO LA KISASA KISUTU ILALA.

Hii ni picha ya soko la kisasa la Kisutu ambapo ujenzi wake unatarajia kuanza hivi karibuni katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akizindua ujenzi wa soko la kisasa la kisutu baada ya kuonyesha  picha ya soko hilo  
Wafanyabishara wa soko la kisutu wakishangilia uzinduzi wa soko la kisasa.
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Serikali ya Awamu ya tano imetenga bilioni 16 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la Kisutu lililopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ambalo litachukua wafanyabiashara zaidi ya 1,500.

Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa soko hilo leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema, amesema kuwa ujenzi soko hilo litatejegwa kwa muda wa miezi 18 kunzia april 15 mwaka huu.

Amesema kuwa soko hilo litakuwa na gorofa nne ambazo zitawapa fursa wafanyabiashara kupata huduma muhimu ikiwemo huduma za kibenki, eneo la maegesho ya magari, mabucha, machinjio pamoja na vyoo vya umma.

Mhe. Mjema ameeleza kuwa tayari Manispaa ya Ilala imepokea bilioni 2 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa ujenzi wa soko la kisasa.

“Wakati umefika wafanyabiashara wa Kisutu kufanya biashara katika mazingira rafiki, kwani muda mrefu walikuwa wanapata shida baada mvua kunyesha….Rais John Magufuli ataendelea kuleta maendeleo” amesema Mhe. Mjema.

Hata hivyo amesema kuwa mkandarasi tayari amepatikana na kazi iliyopo mbele yao ni kusimamia utekelezaji wa ujenzi ili ukamilike kwa wakati kama ulivyokusudiwa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela, amesema kuwa jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Ilala zimezaa matunda kutokana na mafanikio yaliokuwepo kwa sasa.

Amesema kuwa tangu mwaka 1964 soko la kisutu lipo katika mazingira ambayo sio rafiki katika ufanyaji wa biashara.

Palela amesema kuwa baada ya jitihada za Mhe, Mjema wamefanikiwa kupata soko la kisasa ambalo litaweza kuwa na wafanyabiashara zaidi ya 1,500.

“Kipindi cha nyuma soko la kisutu lilikuwa linaitwa ‘Soko Mjinga’ lakini kutokana na jitihada za serikali tuona maboresha makubwa kwa kujenga soko la kisasa” amesema Palela.

Mwenyekiti wa Soko la Kisutu Zuberi Luono, amesema kuwa kujengwa kwa soko la kisasa ni mafanikio kwao kwani soko hilo litawapa fursa kuwa idadi kubwa ya wafanyabiashara tofauti na awali.

Amesema kuwa wafanyabiashara wanaendelea kuishukuru serikali kwa kuwapa ushirikiano katika kuwasaidia kwa kuwajengea soko la kisasa.

Kutokana na ujenzi wa soko la kisasa la kisutu wafanyabiashara 633 watapisha ujenzi wa soko na kupelekwa kufanya biashara katika eneo la mkunguni na stendi ya zamani ya kisutu.

Kabla ya kuhamia katika maeneo hayo, Manispaa ya Ilala itatumia milioni 138 kwa ajili ya gharama za ujenzi wa masoko hayo mawili kwa ajili ya ujenzi na maboresho.

Ujenzi huo ni nyumba za machinjio, miundombinu pamoja na mabanda katika maeneo yote mawili.

No comments