MWADUI YAJINUSURU KUSHUKA DARAJA DHIDI YA MBAO FC
Ligi Kuu Bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika Uwanja wa Mwadui Complex kwa Mwadui ikikaribisha Mbao FC.
Mchezo uliopigwa majira ya saa kumi ulimalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Charles na Ilanfya katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza na kuweza kudumu dakika 90 zote za mpambano huo.
Matokeo hayo yanainusuru Mwadui kujiweka katika mazingira ya kutoshuka daraja baada ya kupata alama tatu muhimu na kufikisha jumla ya pointi 29 ikipanda mpaka nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi.
Post a Comment