Ads

FURSA YA ASILIMIA 70 YA UWEKEZAJI YABAINIKA KIGAMBONI.

IMG_20180409_104931
 Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji Manispaa ya Kigamboni Dotto Msawa akifatiwa na Afisa Mipango Miji Manispaa ya Kigamboni Nice William
IMG_20180409_110419
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa, akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam

MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKAUGA, DAR ES SALAAM
Wadau mbalimbali nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika Wilaya ya Kigamboni ambapo kuna asilimia 70 ya maeneo ambayo hayaendelezwa kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Akizugumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa, amesema kuwa kigamboni bado kuna maeneo rafiki kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo viwanja vya ufukweni.

Amesema kuwa tayari wametenga maeneo ya uwekezaji ikiwemo viwanda, kwani baada ya kufanya operesheni imebainika bado kuna fursa ya asilimia 70 kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.

Mgandilwa amewataka watu wote ambao wanamiliki maeneo ya ufukweni katika wilaya hiyo, kufanya uwekezaji kama ilivyokusudiwa ili serikali iweze kukusanya kodi kwa ajili ya ujenzi wa taifa.

“Kuna wakazi wa kigamboni maeneo ya ufukweni wamefanya makazi badala ya kufanya uwekezaji…natoa muda wa mwezi mmoja ili waweze kufanya uwekezaji, kama wakishindwa tutapendekeza viwanja waviache” amesema Mgandilwa.

Ameeleza kuna watu wengi wanaoyesha nia ya uwekezaji katika maeneo ya ufukweni, lakini kuna baadhi wemekaa nayo maeneo hayo kwa muda mrefu ila kuyaendeleza.

“Serikali inaitaji kodi, unapokaa eneo la uwekezaji bila kuliendeleza ni kuikosesha mapato” amesema Mgandilwa.

Aidha ameeleza kuwa wakazi wote wilaya ya kigamboni wanatakiwa kuomba vibali kabla ya kujenga ili kuepuka kujenga katika maeneo ambayo sio rasmi.

Afisa Mipango Miji Manispaa ya Kigamboni Nice William, amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa kila mkazi wa wilaya hiyo hasa katika kujenga kwa kufata taratibu.

“Tumejipanga kuendeleza mji wa kigamboni ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira rafiki” amesema William.

Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji Manispaa ya Kigamboni Dotto Msawa, amesema kuwa wakati umefika wawekezaji kuwekeza kigamboni kutokana kuna mazingira rafiki.
Amesema kuwa mpaka sasa ni asilimia 30 ambayo imetumika katika uwekezaji katika wilaya hiyo, huku akieleza kuwa wamejipanga kufaya maboresho ili kuhakikisha kuna kuwa na vyazo vingi vya mapato

No comments