MAKONDA, IGP SIRO WATEULIWA KAMATI ZA MAANDALIZI AFCON U17.
Wakati Makonda,
ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Abubakar Bakhresa
ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Usafiri na
Malazi.
Uteuzi huo umefanywa
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais wake, Wallace Karia
na Makonda atasaidiwa na Makamu Mwenyekiti, Yusuph Singo ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Michezo, Wajumbe Sunday Kayuni, Leslie Liunda, Nassoro
Idrissa ‘Father’, Mohamed Kiganja ambaye ni Katibu wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) na Mhandisi Davis Shemangale.
Bakhresa atakuwa
chini ya Mwenyekiti Mhandisi Ladislaus Matindi na Wajumbe Aziz Abood,
Ahmed Mgoyi, Ahmed Shabiby, Dk. Maige Mwakasege Mwasimba na Shebe
Machumani.
TFF pia imeunda
Kamati ya Masoko na Habari chini ya Mwenyekiti, Kelvin Twissa na Wajumbe
Mwandishi wa Habari za Michezo na Katibu wa zamani wa TFF, Angetile
Osiah, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas, Dk.
Omari Swaleh wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mkurugenzi wa AMG Group Iman
Kajula na Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando.
Kamati nyingine ni ya
Fedha na Mipango itakayokuwa chini ya Mwenyekiti, Doto James na Wajumbe
Mohamed Dewji, Dk. Seif Muba, Bernard Lubogo, Paul Bilabaye,
Jacquelline Woiso na Cornel Barnabas.
Kamati ya Uratibu
Utalii itakuwa chini ya Mwenyekiti, Dk Khamis Kigwangala na Wajumbe ,
Allan Kijazi Devotha Mdachi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya
Temeke, Hoyce Temu, Leah Kihumbi ambaye ni Mkurugenzi wa Sanaa na
Makamu Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani.
Kamati ya Itifaki,
Mwenyekiti ni Mndolwa Yusuph ambaye ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na
Wajumbe Filbert Bayi, Mkurugenzi Uwanja wa Ndege JNIA, Happiness
Luangisa, Alex Makoye Nkenyenge na Alhaji Idd Mshangama.
Kamati ya Tiba na
Udhibiti wa Dawa za Kusisimua Misuli itakuwa chini ya Mwenyekiti,
Profesa Lawrence Museru, Dk. Paul Marealle, Dk. Edmund Ndalama, Dk.
Christina Luambano, Daktari Mkuu wa Hospitali ya Temeke na Hiiti Sillo.
Kamati ya Sheria na Taratibu Mwenyekiti ni William Erio na Wajumbe Dk. Damas Ndumbaro, Edwin Kidifu, Ally Mayai na Khalid Abeid.
Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mwenyekiti ni IGP Simon Siro na Wajumbe Michael Wambura, CP.
Andengenye wa Zimamoto, CP. Lazaro Mambosasa wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar-es-Salaam, Mkuu wa Askari wa Usalama Barabarani, TISS na Jonas
Mahanga.
Kamati ya Rasilimali
Watu itakuwa chini ya Mwenyekiti Dk. Francis Michael, Allan Kijazi, Wane
Mkisi, Juliana Yassoda na Gerald Mwanilwa.
Kamati hizo ndogo
zitakuwa chini ya Kamati Kuu inayoongozwa na Mwenyekiti Dk. Harrison
Mwakyembe (MP); Makamu Mwenyekiti wa Leodegar Tenga na Mtendaji Mkuu wa
Kamati hiyo ni Henry B. Tandau.
Post a Comment