Arsene Wenger anatamka mkufunzi wa Feyenoord Giovanni van Bronckhorst kuwa mrithi wake kama mkufunzi wa Arsenal.
Real Madrid wanatumai wataishinda Manchester City katika kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28.
Image captionAlexi Sanchez
Paris St-Germain huenda ikamtaka Sanchez katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Chile ikitarajiwa mwishoni mwa msimu.
Everton hawana matumaini tena ya kumsajili mkufunzi wa Warford Marco Silva kama mkufunzi wake mpya.
The Toffees wanataka kumuajiri mkurugenzi wa michezo wa klabu ya RB Lipzig Ralf Rangnick badala yake.
Image captionSam Allardyce
West Brom huenda wakafeli katika harakati zao za kutaka kumuajiri Sam Allardyce kama mkufunzi wake mpya.Mkufunzi huyo ana hamu ya kurudi kufunza timu za kimataifa.
Mkufunzi wa klabu ya Hull Leonid Slutsky anajaribu kuokoa kazi yake baada ya klabu hiyo kurekodi matokeo mabaya katika ligi hiyo ya mabingwa.
Image captionDelle Ali na Harry Kane
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 24, na kiungo wa kati Dele Alli, 21, ni miongoni mwa wachezaji watano wanaosakwa na rais wa klabu hiyo Florentino Perez. (Diario Gol, via Daily Mail)
Manchester City wanapanga kumnunua winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 26. (Don Balon, kupitia Manchester Evening News)
Image captionAhmed Musa wa Nigeria
The Foxes watamuuza mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa, 25,mshambuliaji wa Argentina Leonardo Ulloa, 31, pamoja na beki wa Tunisia Yohan Benalouane, 30, mnamo mwezi Januari.
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amezuia hatua ya klabu hiyo kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 29. (Diario Gol, via Daily Star)
Image captionJulian Draxler wa Ujerumani na PSG
Liverpool imewasiliana na PSG kuhusu uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24.
Mkufunzi wa zamani wa West Ham, Newcastle na Crystal Palace boss Alan Pardew ndio anayepigiwa upato kumrithi Tony Pulis katika klabu ya West Brom.
Image captionArsenal huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ureno Joao Mario
Arsenal huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ureno Joao Mario kwa kitita cha £26m mnmao mwezi Januari.
Sampdoria haitamuuza kiungo wake wa kati mwenye umri wa miaka 21 Lucas Totteira kueleka Everton mwezi Januari.
Mchezaji anayelengwa na Manchester City Joshua Kimmich, kiungo wa kati mwenye umri wa 22 kutoka Ujerumani anaendelea na majadiliano na klabu yake ya sasa Bayern Munich.
Liverpool na Tottenham ni miongoni mwa vilabu vinavyomsaka kinda wa timu ya Stevenage katika ligi ya daraja la pili ya Uingereza Ben Wilmot.
Post a Comment