MBIVU NA MBICHI ZA UCHAGUZI JUMUIYA YA WAZAZI CCM DAR KUJULIKANA LEO
Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nani ya Nchi, Hamad Massauni
amewapongeza madiwani waliofanya vizuri katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani
uliomalizika hivi karibuni katika baadhi ya mikoa.
Pongezi hizo
amezitoa leo jijijini Dar es Salaam wakati akifungua Uchaguzi wa Viongozi wa
Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho wa mkoa huo.
Amesema kutokana na sera madhubuti za CCM zlizotolewa kipindi cha kampeni kwa kiasi kikubwa zimechangia wananchi kushawishika kuwapigia kura wagombea waliofanikisha chama hicho kupata ushindi mnono.
“ Naomba
niwapongeze viongozi waliomaliza muda katika nafasi mbalimbali pia kwa kile
kipigo cha mbwa nawapongeza madiwani walioshiriki uchaguzi katika kata
takribani 43,” amesema.
Massauni amesema mshikamano na ushirikano
ulionyeshwa na viongozi katika mchakato mzima uchaguzi umechangia chama hicho
kupata ushindi wa kishindo.
Amesisisitiza kuwa kutokana na utendaji madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo kupambana na rushwa, ubadhirifu, matumizi mabayaya madaraka, matumzi mabaya ya rasilimali za umma huku akiongeza kuwa utendaji huo umesbababisha wapinzani kukosa ajenda.
Ameafafanua
kuwa Rais John Magufuli ametekeleza ilani ya vyema ilani ya CCM na kwamba
maalalmiko ya wananchi yaliyokuwa yakiwasilishwa Serikalini yamepungua
ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Aidha,
amesema chama hicho kilipoteza majimbo katika mkoa huo kutokana na baadhi ya
wanachama wasaliti kukisaliti chama na kwamba wasaliti hao wameshaghulikiwa na
ngazi husika.
Amewataka
wagombea wanaoshiriki uchaguzi huo kuzitendea haki nafasi zao endapo watapata
fursa ya kupigiwa kura na wajumbe huku
akibainisha nafasi wanazozigombea.
Kwa upande
wake mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa wazazi wa jumuiya hiyo mkoani humo,
Frank Kamugisha ,amesema endapo
atachaguliwa atakeleza vyema ilani ya chama pamoja na malengo ya kuwepo jumuiya
hiyo.
Pia amesema
chama hicho hakijawahi kushindwa katika jimbo lolote ila matokeo ya kushindwa
husababishwa na mifarakano na migogoro baina ya wanachama.
Amewapaongeza
wapinzani waliojiunga na chama hicho
kwani wameonyesha kujitambua na nia ya dhati kuiletea nchi maendeleo kwa
kushirikiana na chama tawala.




Post a Comment