SIMBA B YAICHAPA 4 KIKOSI CHA WABUNGE.
Kocha mkuu timu ya vijana Simba B, Musaa Hassan 'Mgosi' akiwanoa vijana wake leo katika Viwanja vya JK Park, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mshambuliaji wa Zamani wa Simba ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya vijana ya Simba ‘Simba B’, Mussa Hassan ‘Mgosi’, leo Jumatano alikuwa bize akiendelea kuwanoa vijana wa kikosi hicho kwenye Viwanja vya JK Park, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mgosi ambaye alikuwa meneja wa timu ya wakubwa kabla ya baadaye kubadilishiwa majukumu aliongoza mazoezi ya vijana hao ambapo baadaye pia aliongoza kikosi hicho kushinda mabao 4-0 dhidi ya timu ya Wabunge wa Tanzania, Bunge Sports Club kwenye uwanja huo kwenye mchezo wa kirafiki

Post a Comment