Ads

DK. SHIKA NDANI YA USIKU WA 900 ITAPENDEZA DAR LIVE MBAGALA.

Mwambawahabari

 Meneja wa Dk Shika Catherine Kahabi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


 Dk Shika (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam's kufika katika hafla hiyo.

Na Maria Kaira,Mwambawahabari



Dk  Shika anatarajia kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es salaam siku ya Desemba 9 mwaka huu, katika hafla ya usiku wa 900 Itapendeza itakayofanyika katika ukumbi wa Dar live Mbagala ambapo ataongea na kuelezea historia yake alipotoka na alipo kwa sasa.



Akizungumza na waandishi wa habari Leo Meneja wa  Dk Shika   Catherine Kahabi, amesema Dk.Shika  ni miongoni mwa watu waliojipatia umaarufu  mkubwa kwa muda mfupi kutokana na kushinda mnada wa nyumba za Tajiri Lugumi na kuweza kumweka katika muonekano wa ubilionea.



 " Hafla hii tumeipa jina la Usiku wa 900 Itapendeza kwa lengo La kumtambulisha Dk . Shika kwa wakazi wa Dar es Salaam , waweze kumfahamu zaidi"amesema



Aidha amesema katika hafla hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wakiwemo wachekeshaji, wasanii wa bongo fleva pamoja na bendi mbalimbali zitatumbuiza Sikh hiyo.



Pia amesema Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Masha.

No comments