Wadau wa Tasnia ya filamu jitokezeni kuchangia katika mfuko wa maendeleo ya filamu kusaidia kuinua vipaji – Mhe. Mwakyembe
Mwambawahabari
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) akizungumza wakati wa kikao na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya
filamu kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu
nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi.
Joyce Fissoo
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kulia) akifafanua jambo
wakati wa kikao na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu kujadili namna mfuko
huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe na kushoto ni Katibu Mfuko wa Maendeleo ya Filamu Bibi. Asha
Mtwangi
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kulia) akipokea taarifa ya hatua iliyofikia mfuko wa maendeleo ya filamu
kutoka kwa Katibu wa mfuko huo Bibi. Asha Mtwangi wakati wa kikao na wajumbe wa
mfuko wa maendeleo ya filamu kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na
kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Mfuko wa maendeleo ya filamu Bw. Juma Chikoka (kulia) akichangia mada
wakati wa kikao na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu kujadili namna mfuko
huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya filamu nchini leo Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu
baada ya kikao kujadili namna mfuko huo utakavyokusanya na kuendeleza sekta ya
filamu nchini leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM
Na: Genofeva Matemu
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wanatasnia ya
filamu nchini kujitokeza kwa wingi kuchangia mfuko wa maendeleo ya filamu
ulioanzishwa kwa ajijli ya kukusanya pesa na kutoa mikopo kwa wasanii wa filamu
ili kuendeleza vipaji vya filamu nchini.
Hayo ameyasema Jana
Jijjini Dar es Salaam alipokutana na wajumbe wa mfuko wa maendeleo ya filamu
pamoja na viongozi wa shirikisho la filamu kuzungumza namna mfuko huo
utakavyofanya kazi na kulenga makundi yote ya wanatasnia katika mikoa yote
nchini.
“Wazo la kuanzisha
mfuko huu ni hatua kubwa mno mmechukua pamoja na kujiamini kwani tatizo kubwa
tulilonalo linalokwamisha maendeleo ya filamu ni pamoja na ukosefu wa mitajji
hivyo kuwaingiza vijana wetu katika mikataba ya unyonyaji; naamini mfuko huu
utaondoa kero hiyo na kuboresha maslahi ya tasnia ya filamu nchini” amesema
Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe
amesema kuwa atahakikisha kuwa anapitia mikataba ya wasanii wote ili kuona kama
mikataba wanayoingia kuandaa filamu inaendana na kazi wanazozitoa kwani kwa
kufanya hivyo kutawasaidia wasanii kujitambua na kuingiza kipato halali
kitakachoendana na kazi walizofanya.
Akizungumza katika
kikao hicho Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa
baadhi ya wasanii wamekosa fursa ya kuonyesha vipaji vyao kutokana na ukosefu
wa mitaji au njia elekezi ya kufanisi vipaji vyao, hivyo mfuko wa Maendeleo ya
filamu unalenga kuwafikia wasanii wote kutoka mikoa yote nchini kwani ajira
kwenye filamu haina ukomo wa umri.
Naye Rais wa
Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amempongeza Mhe. Mwakyembe kwa
jitihada anazozionyesha katika kupigania maslahi ya wasanii na kuahidi
kuwahamasisha wanachama wa shirikisho la filamu kuchangia katika mfuko wa
maendeleo ya filamu ili waweze kuinua vipaji na kuleta mapinduzi ya kweli
katika tasnia ya filamu.
Post a Comment