Ads

NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43


 KAZ4


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC  Jaji  Semistocles  Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.
Jaji Kaijage amesema tume imetangaza kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.
Jaji Kaijage ameainisha  kwamba kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.
“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe 26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.
Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.
Jaji Kaijage aliema Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.
Alitoa mwito kwa vyama vya Siasa na Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.
Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:
Zifuatazo ni Kata 43 zitazohusika katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani:
 
Na
 
MKOA
 
HALMASHAURI
 
KATA
1.ARUSHAHalmashauri ya Wilaya ya ArushaMusa
Halmashauri ya Jiji la ArushaMuriet
Halmashauri ya Wilaya ya MeruAmbureni
Halmashauri ya Wilaya ya MeruNgabobo
Halmashauri ya Wilaya ya MeruMaroroni
Halmashauri ya Wilaya ya MeruLeguruki
Halmashauri ya Wilaya ya MeruMakiba
Halmashauri ya Wilaya ya MonduliMoita
2.     2

DAR ES SALAAMHalmashauri ya Manispaa ya KinondoniMbweni
Halmashauri ya Manispaa ya TemekeKijichi
Halmashauri ya Manispaa ya UbungoSaranga
3.DODOMAHalmashauri ya Wilaya ya MpwapwaChipogolo
4.GEITAHalmashauri ya Wilaya ya Nyang’waleBukwimba
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

Senga
5.

IRINGAHalmashauri ya Manispaa ya IringaKitwiru
Halmashauri ya Wilaya ya KiloloKimala
6.

KILIMANJAROHalmashauri ya Manispaa ya MoshiBomambuzi
Halmashauri ya Wilaya ya HaiMnadani
Halmashauri ya Wilaya ya HaiMachame Magharibi
Halmashauri ya Wilaya ya HaiWeruweru
7.LINDIHalmashauri ya Manispaa ya LindiChikonji
Halmashauri ya Wilaya ya RuangwaMnacho
8.

MANYARAHalmashauri ya Wilaya ya Hanang’Nangwa

9.

MBEYAHalmashauri ya Wilaya ya RungweIbighi
10.

MOROGOROHalmashauri ya Wilaya ya MorogoroKiloka
Halmashauri ya Wilaya ya MalinyiSofi
11.MTWARAHalmashauri ya Wilaya ya TandahimbaMilongodi
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara  MikindaniReli
Halmashauri ya Mji wa MasasiChanikanguo

12.MWANZAHalmashauri ya Wilaya ya MisungwiKijima
Halmashauri ya Jiji la MwanzaMhandu
13.RUKWAHalmashauri ya Manispaa ya SumbawangaSumbawanga
14.  14

RUVUMAHalmashauri ya Wilaya ya TunduruLukumbule
Halmashauri ya Wilaya ya TunduruKalulu
Halmashauri ya Wilaya ya MbingaMuongozi
15.SINGIDAHalmashauri ya Wilaya ya IkungiSiuyu
16.SIMIYUHalmashauri ya Wilaya ya MaswaNyabubinza
17.SONGWEHalmashauri ya Wilaya ya MombaNdalambo
18.TABORAHalmashauri ya Wilaya ya NzegaNata
Halmashauri ya Wilaya ya UramboMuungano
19.


TANGAHalmashauri ya Mji wa KorogweMajengo
Halmashauri ya Wilaya ya LushotoLukuza
Halmashauri ya Wilaya ya BumbuliMamba
Imetolewa leo tarehe 04 Oktoba, 2017.

No comments