MISS TANZANIA JULITHA ATAMBA KUFANYA VYEMA KUFANYA VYEMA MISS WORLD 2017.
Mwambawahabari
Mwakilishi wa Tanzania katika
mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete
(katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
kwenye hotel ya Hyatt . Kulia Mkurugenzi wa Lino International Agency
ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga na kushoto ni
Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby
Msammy katika hafla iliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt jijini Dar es
Salaam.

Mwakilishi kutoka wizara ya
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby Msammy (kushoto)
akimkabidhi bendera Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya kumsaka
mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete (katikati) katika
hafla ya kumuaga iliyofanyika jana kwenye hotel ya Hyatt . Kulia
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss
Tanzania, Hashim Lundenga.

Mwakilishi wa Tanzania katika
mashindano ya kumsaka mrembo wa Dunia, Miss World 2017, Julitha Kabete
akiwa katika pozi mara baada ya kukabidhiwa bendera kwenye halfa fupi
iliyofanyika kwenye hotel ya Hyatt
………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Miss World
Tanzania, Julitha Kabete (21) ametamba kufanya vyema katika mashindano
ya 67 ya kumsaka mrembo ya Dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Sanya,
nchini China mwezi ujao.
Julitha ambaye anaondoka leo,
amesema kuwa amejiandaa vyema ili kuiletea sifa Tanzania katika
mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Novemba 18 kwenye ukumbi wa Sanya
City Arena in Sanya, China PR.
Stephanie na kushirikisha jumla
ya warembo 120. Julitha anaondoka leo kwenda China chini ya udhamini wa
Turkish Airline. Mrembo huyo aliagwa na kukabidhiwa bendera na
Mwakilishi kutoka wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Habiby
Msammy katika hafla iliyofanyika kwenye Hotel ya Hyatt jijini Dar es
Salaam.
“Nimejiandaa vizuri katika
mashindano haya, nina uzoefu mkubwa kwani nilishinda mashindano ya Miss
Dar City Center, Miss Ilala na kwenye fainali za miss Tanzania 2016
ambako niliingia tano bora. Pia nilishiriki mashindano ya Afrika na
kufanya vyema,” alisema Julitha.
Mkurugenzi wa Lino International
Agency ambao ndiyo waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema
Julitha ni mrembo wa 23 kuiwakilisha nchi kwenye Miss World.
“Mwaka huu shindano la Miss
Tanzania limechelewa kufanyika, hivyo tukaamua kumtea Julitha
akatuwakilishe kwenye Miss World, uteuzi wake umezingatia vigezo vyote
na hakuna shaka atafanya vizuri katika fainali hizo ambazo tumekuwa na
rekodi ya kutwaa taji la Miss World Afrika na mataji mengine,” alisema
Lundenga.
Mrembo huyo aliondoka nchini jana
usiku kuelekea katika kambi ya Miss World nchini China ambapo atachuana
na warembo wengine kutoka mataifa zaidi ya 120 kusaka mshindi katika
fainali itakayofanyika baadae Novemba nchini humo.
Post a Comment