MANISPAA YA ILALA YAFANYA USAFI KATIKA MAENEO KOROFI YA UFUKWENI
![]() |
| Baadhi ya Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakifanya usafi. |
mwambawahabari
Na Noel Rukanuga
Na Noel Rukanuga
Viongozi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo wamefanya usafi
katika fukwe ya bandari ya Dar es Salaam ambayo imeonekana ni korofi kutokana
na uchavu mwingi uliokuwepo katika fukwe hiyo iliyopo Kata ya Kivukoni.
Usafi huo ni sehemu ya
utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. John Pombe Magufuri ambapo kila juma mossi ya mwisho wa mwezi huwa
wanafanya usafi hasa katika maeneo ambayo yameonekana Kuwa na uchavi mwingi.
![]() |
| Vijana wa Palepale Jogging wakifanya usafi |
Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Ilala Bernadeter Mwaikambo, amesema kuwa wamekuwa wakifanya usafi
huo kila juma mossi ya mwisho wa mwezi kwa ajili ya kuhakikisha maeneo yote
ndani ya manispaa hiyo yanakuwa katika hali ya usafi.
Mwaikambo amesema
wataendelea kutoa elimu kwa kushirikiana na wenyeviti wa Serikali za mtaa ambao
wameonekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi katika kufanikisha suala la
kusafisha mazingira linafanikiwa.
![]() |
| Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala akiwa katika harakati za kufanya usafi. |
![]() |
| Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Bernadeter Mwaikambo akifanya usafi. |
Amewashukuru watu wote waliojumuika kufanya
usafi huku akibaisha kuwa halmashauri imejipanga kuweka mazingira kuwa masafi
muda wote.
“Si mpaka kufanya usafi tusubiri mwisho wa
mwezi, kwani mikakati tuliyonayo kwa sasa ni kuendelea kutoa
elimu kwa wananchi na kuhakikisha takataka zinazolewa kwa wakati” amesema
Amewataka viongozi wa siasa kuendelea kuhamasisha
jamii kwa nguvu kuhusu kufanya usafi katika maeno yote ndani ya manispaa hiyo.
![]() |
| Mkuu wa kitengo cha Idala ya Mazingira Manispaa ya Ilala Abdon Mapunda akifeka majani |
Mkuu wa kitengo cha Idala ya Mazingira Manispaa ya Ilala Abdon
Mapunda amesema kuwa mazingura kuwa safi ni jambo la muhimu sana kwa
binadamu.
Ameesema wameamua kufanya usafi kwenye ufukwe huo kwa sababu
maeneo hayo mara nyingi yamekuwa yakisahaulika licha ya kuwa ni makazi kwa
baadhi ya watanzania wanaoishi kwenye mazingira magumu.
"Usafi
wa mazingira ni jambo muhimu sana kwenye mazingira ya binadamu hivyo ni lazima
kufanya usafi kwenye mazingira yanayotuzunguka” amesema Mapunda.
Mwenyekiti wa Chama Cha Vijana cha Jogging amesema kuwa vijana wanapaswa kujitokeze
kwa wingi kufanya usafi kwenye maeneo yao yanayowazunguka na wasione kama
wanaonewa na serikali kwani ni wajibu wao kufanya hivyo.
Joseph
Amir mkazi wa eneo hilo laufukweni amesema kuwa eneo hilolimeonekana kuwa
sugu kwa kuwa na takataka nyingi kwa sababu ya watu kutokuwa na uelewa juu ya
kutuza mazingira.
Amesema kuwa ni vema serikali ikatoa adhabu Kali kwa wafanyabiashara
wadowadogo wanaolizunguka eneo hilo kwani wao ndio ufanya vitendo hivyo vya
kutupa taka ovyo pembezoni mwa bahari.





Post a Comment