JAFO AWAPA PONGEZI WANANCHI WA KISARAWE
Mwambawahabari
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa Ofisi ya walimu iliyojengwa kisasa katika shule ya msingi Kwala wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiipongeza kamati ya ujenzi kijiji cha Kwala wilayani Kisarawe kwa ujenzi wa madarasa mapya.
Baashi ya matundu ya vyoo yaliyokamilika kujengwa wilayani Kisarawe.
Diwani wa kata ya Mzenga Mohamed Lubondo(katikati) akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Mitengwe wilayani Kisarawe.
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Mitengwe wilayani Kisarawe.
………………….
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewapongeza wananchi wa kisarawe kwa ushirikiano mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, Ofisi za walimu, nyumba, pamoja na vyoo.
Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akikagua mradi ya ujenzi wa madarasa wilayani kisarawe katika vijiji vya Mitengwe, Kitonga, Boga, na kwala.
Katika vijiji hivyo, Jafo alikagua ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 15, Ofisi za walimu 4, pamoja na matundu ya vyoo 40 ambapo ujenzi wake unafanyika kwa bora unaotakiwa.
Kutokana na mwamko mkubwa ulioonyeshwa na wananchi hao katika kushirikiana na serikali na viongozi walio wachagua akiwemo mbunge na madiwani wote wa kisarawe, Jafo amesisitiza wananchi wengine katika wilaya mbalimbali kushirikiana na serikali pamoja na viongozi wao ili kujiletea maendeleo
Post a Comment