Ads

SERIKALI ZA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI ZASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA KUTEKELEZA PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

Mwambawahabari

01
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisaini Mkataba wa Makubaliano kati ya Tanzania na Afrika Kusini wa namna ya kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kwa lengo la kukusanya, kuhifadhi, kuendeleza na kuzitunza urithi huo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017. Kushoto ni Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwa.
03
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akibadilishana Mkataba wa makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika na  Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwa mara baada ya kusaini mkataba huo mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017.
04
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na viongozi kutoka Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017.
05
Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiongea na viongozi kutoka Tanzania na Afrika Kusini waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma.
06
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitambulisha wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika mjini Dodoma.
07
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Tanzania Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpokea mgeni wake Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthethwaalipowasili Uwanja wa ndege mjini Dodoma jana Tarehe 19 Septemba 2017. Zizra hiyo inalengo la kusaini Mkataba wa Makubaliano wa kutekeleza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara kati ya Afrika Tanzania na Afrika Kusini.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)

No comments