Ads

POLISI YATOA UFAFANUZI JUU TA VIFO VYA WATOTO WALIOLIPUKIWA NA BOMO MKOANI ARUSHA.

Mwambawahabari 

Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amewataka viongozi waliopo karibu na kambi za mazoezi ya kijeshi kuweka utaratibu wa kuwakumbusha wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitu wasivyovijua hasa vyenye asili ya chuma ili kuepusha madhara.
Kamanda Mkumbo ametoa hadhari hiyo alipokuwa akizungumzia tukio la vifo vya watoto watatu wakazi wa kata ya Loksale wilayani Monduli vilivyosababishwa na mlipuko wa bomu walilookota wakati wanachunga mifugo na kuanza kulichezea kama mpira ambalo lililipuka na kuwajeruhi vibaya miguuni.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda Mkumbo amesema licha ya kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya lakini lingeweza kuepukika kama watoto hao wangeweza kutoa taarifa ya kitu walichokiona.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa watoto hao wangewezakufanya hivyo kama wangekuwa wanakumbushwana wazazi wao mara kwa mara wanapokwenda machungani.
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Monduli Bw. Iddy Kimanta aliyezungumza na ITV kwa njia ya Simu amesema watoto hao wote ni wanafunzi wa shule ya msingiNafko na wawili akiwemo Landisi Setabau miaka 12 na Samweli Nyandusi miaka 9 walikuwa wanasoma darasa la kwanza wakati mwingine aliyetajwa kwa jina la Seuri Losila miaka alikuwa darasa la tatu.
Viongozi wa eneo lililopotokea tukio hilo wamesema kimsingi tukio hiloni bahati mbaya kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakielimishwa juuya kufuata maelekezo na mara nyingi wamekuwa wakitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja kutoa taarifa wanapoona mabaki ya vyuma.
Kwa mujibu wa viongozi hao katika maeneo mengi ya wafugaji wakati wa likizo watoto huwasaidia wazazi wao kuchunga mifugo na pia wakati wote wamekuwa wakitoa taarifa wanapokutanana vitu kama hivyo na wahusika wamekuwa wakifikamara moja na kuvichukua.

No comments