Ads

MAKONDA ATOA AGIZO , BILION 6 MKOA WA DAR ES SALAAM , KUKOPESHWA KWA WAFANYABIASHARA WADOGO.

Mwambawahabari
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe. Paul Makonda amezielekeza manispaa zote za mkoa huo  kutoa mikopo nafuu kwa wajasilimali wenye viwanda vidogovidogo   ili kuweza kusaidia katika uanzishwaji wa viwanda  mkoani humo. 

Makonda amewataka Wafanyabiashara hao kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuonana na Afisa Biashara wakiwa na Mchanganuo wa Biashara zao kisha kueleza kiwango cha Fedha wanazotaka kukuza Biashara zao na kuongeza uzalishaji.

Amesema kuwa amefanya mzungumzo na  mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF  ilikuweza kutoa mikopo nafuu na kusaidi wafanya biashara katika kuanzisha viwanda vidogovidogo na kuwa taka wafanya biashara  hao kufika ofisi ya mkoa  kujiandisha ili wapewe mkopo huo.

 Mheshimiwa Makonda  amesema lengo la Mpango huo ni kuwawezesha Wafanyabiashara kuwa na Mitaji itakayowafanya kukuza Viwanda vyao ili kufikia malengo na azma ya  Rais DR.John Magufuli  ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Katika juhudi za kuwakwamua Wafanyabiashara wazawa  Makonda ameeleza  mpango wa kuanzisha Soko la kuonyesha na kuuza bidhaa zinazozalishwa na wazawa kila Mwezi mara Moja kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Hata hivyo  Makonda amezielekeza Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam  kuhakikisha 10% ya fedha zinazotengwa kwaajili ya kuwakopesha  Kinamama, Vijana na Walemavu zinatolewa kwa Wafanyabiashara wenye Viwanda Vidogovidogo  ili kuwaongezea nguvu na kwamba katika mkoa huo jumla ya shilingi bilion 6 zipo kwaajili ya walengwa.

Katika hatua nyingine  RC Makonda  amewataka  Wamachinga kutoa kipaombele kwa kuuza Bidhaa zinazozalishwa na Wafanyabiashara wazawa  ilikukuza uchumi wa Tanzania.

No comments