M-KOPA YATOA MSAADA WA MITAMBO YA SOLA MASHULENI
Mwambawahabari
M-KOPA imetoa msaada wa mitambo ya sola kwenda
shule ya sekondari Isandula iliyopo wilaya ya Mbozi. Msaada huu una nia ya
kuwezesha wanafunzi kujisomea vizuri na kwa uhuru nyakati za usiku.
Huu ni msaada wa pili mwaka huu, baada ya M-KOPA
kutoa msaada kama huo shule ya sekondari Mwinyi iliyopo Mkuranga, Pwani. Kukosa
mwanga salama wakati wa usiku kumepelekea wanafunzi kutumia njia hatarishi kama
vibatari na mishuma, inayo athiri afya zao na kupunguza muda wa kujisomea.
Richard Machera, Meneja Mauzo M-KOPA alisema, “Tumeona changamoto…. Watoto wa shule
wanazopitia wakiwa wanajisomea na kufanya soma ya ziada. Mradi huu wa kijamii
utasaidia kutatua changamoto za mwanga kwa shule zilizo nje ya umeme wa gridi
ya taifa”.
Utafiti uliofanywa na M-KOPA unaonyesha kuwa 92%
ya wateja wake wamefaidika na bidhaa za sola kwa kusaidia kuwezesha watoto
kujisomea nyakati za usiku na kupelekea maendeleo mazuri ya matokeo yao ya
mtihani.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Isandula, Bw.
Witson Mtafya asema, “Tungependa
kuishukuru M-KOPA kwa msaada huu waliotupa. Nina imani kuwa wanafunzi wateweza
kupata muda wa ziada wa kujisomea na kufanya mijadala kwenye vikundi kwa fanisi
zaidi na hatimae ufaulu wao kuongezeka”
Msaada uliotolewa unagharimu Tsh. 4,959,000 zikiwemo taa za LED sola 36, chaja za simu, Betri za
kuhifadhi nguvu ya sola 9, paneli 9, tochi 9 na redio za kisasa za sola 9.
Mitambo hii imefungwa kwenye madarasa mawili, ofisi za mwalimu mkuu na mwalimu
mkuu msaidizi na mabweni mawili. M-KOPA sola inaendelea kutoa misaada zaidi
kama hii kwa shule nyingine nchini.
M-KOPA ni kampuni ya
kimataifa inayoongoza kutoa huduma za sola kwenye mfumo wa ‘pay-as-you-go' kwa
nyumba zisizo kwenye gridi. Kampuni hii imeanzisha njia bora Zaidi ya kutoa
huduma nafuu, salama na nishati safi kwa mabilioni ya watu wanaishi sehemu
zisizo na umeme wa gridi ya taifa. Asante kwa mwanga wa jua na technolojia ya
simu, wateja wanaweza kupata mwanga majumbani, kuchaji simu na kusikiliza
redio. Wanaweza kufanya haya yote kwa kuwasha tu swichi na kwa gharama nafuu
Zaidi ya waliyokuwa watumia kwenye mafuta ya taa.
M-KOPA imeshinda tuzo ya
Ubora na Teknolojia kwenye tuzo za FT/IFC Sustainable Finance Awards 2013.
Ilipata tuzo ya Bloomberg New Energy Finance Award 2014. M-KOPA ilitambuliwa
kama kampuni ya nishati safi ambayo ni mfano wa kuigwa mwaka 2014 kwenye Global
Cleantech 100 List na ilikuwa washindi wa kitengo cha SME mwaka 2015 kwenye
Zayed Future Energy Prize.
Post a Comment