BENKI YA CRDB YATOA MILLION 200 KUMUUNGA MKONO RC MAKONDA UJENZI WA OFISI ZA WALIMU
Mwambawahabari
![INDI1](http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/09/INDI1.jpg)
………………………………………………………………………
Bank ya CRDB imemuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kwenye kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za kisasa za Walimu kwa kutoa kiasi cha Shillingi Million 200 ambapo leo wameanza kwa kukabidhi hundi ya Shillingi Million 100 kati ya 200.
Akipokea hundi hiyo RC Makonda amesema Fedha hizo zitasaidia kununua Mifuko 20,000 ya Saruji itakayosaidia kufyatua Matofali 560,000 ambayo yatajenga Ofisi 88 za walimu.
Ameishukuru Bank ya CRDB kwa kuamua kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo ya kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira mazuri yatakayowapa Morali ya kufundisha.
“Kazi yangu ni kumsaidia Rais kupunguza au kuondoa changomoto zilizopo ndani ya Mkoa na sio kuwa mzigo kwa Rais, tayari Rais Magufuli ameshatuonyesha njia katika Sekta ya Elimu alipoamua kutoa Elimu Bure kuanzia Msingi hadi Sekondari kwa lengo la kuwawezesha wanyonge kupata Elimu, kwa tendo hilo limetupelekea sisi Wasaidizi wake kuona tuna wajibu wa kutatua changamoto kwenye Sekta ya Elimu, imekuwa ni ndoto yangu kumuona Mwalimu anathaminika ndio maana pale mwanzoni niliwapambania Walimu wasafiri Bure kwenye Daladala na Treni na sasa tumehamia kwenye ujenzi wa ofisi za walimu” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bank ya CRDB DR. Charles Kimei amempongeza RC Makonda kwa kuwa mbunifu na mwenye mawazo chanya ya kuwasaidia Wananchi hususani Wanyonge na kueleza kuwa wataendelea kumuunga kwenye kila jambo kwakuwa kila fedha wanayoitoa inafanya kazi iliyokusudiwa.
Post a Comment