Ads

WIKI YA SAYANSI AFRIKA ,ILIVYO FANYIKA KATIKA SHULE YA ALMUNTAZIR


mwambawahabari 
Na John Luhende
Mkurugenzi wa shule za Almuntazir Mahamod Ladak , akizungumza na wanafunzi walio shiriki katika wiki ya sayansi shuleni hapo  mzoezi ya kisayansi yame andaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Inspire kwa kushirikiana na taasisi ya NEF , na kudhaminiwa na shule ya Almuntazir, jumla ya shule zipatazo kumi zimeshiriki  zoezi hilo. 

Mkurugenzi wa  shule za Almuntazir Mahamod Ladak akiweka mambo sawa kabla ya wanafunzi kuanza mazoezi ya kisayansi katika shule ya Almuntazil upanga jijini Dar es salaam


 Wanafunzi kutoka shule mbalimbali jijini Dar es salaam wakiwa tayari kuanza zoezi la kisayansi  katika kuadhimisha siku ya Sayansi Africa

wanafunzi wakifanya jaribio la kisayansi  kama walivyo elekezwa na walimu wao 


Wanafunzi  wakiendelea na mazoezi  ya kisayansi
Wanaunzi wa shule ya Almuntazir wakiwa katika picha baada ya kumaliza zoezi la kisayansi  katika maadhimsho ya siku ya Sayansi Afrika 


Wanaunzi wa shule ya Almuntazir wakiwa katika picha baada ya kumaliza zoezi la kisayansi  katika maadhimsho ya siku ya Sayansi Afrika 


wanafunzi wakifanya jaribio la kisayansi  , wana chanya kemikal za kisayansi , ,katika maadhimisho ya siku ya  Sayansi yaliyo fanyika katika shule ya Almuntazir  Upanga jijini Dar es salaam
(Picha na Mpiga picha maalumu  mwambawahabari blog)

 Taasisi mbalimbali kwa kushirikiana na uongozi wa umoja wa shule ya Almuntazir kwa pamoja wameandaa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi yenye kuwasaidia katika kuhakikisha kuwa wanalipenda somo la sience

Akizungumza na vyombo vya habari leo hii mkurugenzi mkuu  wa shule ya Almuntazir Mahmud Ladack Amesema kuwa lengo lao ni katika kuhakikisha wanashirikiana na serikali yote ya hapa nchini katika kuinua wigo mzuri wa elimu hususani kwa wanafunzi wa hapa nchini kujifunza na kuwa na wigo mpana zaidi kwenye masomo ya kisayansi mafunzo hayo ya wanafunzi yaliyofanyika katika shule hiyo ya Almuntazir na yameanaliwa na taasisi ya Nef huku yakilenga katika kuwainua waafrika hususani wanafunzi kuanzia ngazi ya utotot katika kulipenda na kulielewa zaidi somo la kisayansi jambo ambalo litawaweka msatari wa mbele wa kuja kuwa wanasayansi wazuri zaidi kwa mbeleni


Pia ameongeza kuwa lengo lao ni katika kuhakikisha wanafunzi wanlielewa na kulipenda vizuri somo la science ndio maana wao kwa kushirikiana na taasisi ya science project walipoamua kuketi chini na kupata jibu kuwa ili katika kuongeza ufanisi kwa wanfunzi wa shule za msingi katika kuwasaidia kulipenda na kulielewa vizuri somo la science ni vyema wakaandaa siku maalumu ya leo ili wanafunzi wote waweze kukutana na kubadilishana mawazo pamoja na kuwasaidia klatika kujijenga na kuwafanya wayapende masomo ya science kwa pamoja

Naye mwakilishi kutoka science project bi Aneth wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari amesema kuwa wamepata wanafunzi wengi waliojitokeza kwa wingi hususani katika kuja kujifunza kwa vitendo baadhi ya maswala ya kisayansi jambo ambalo wao wanaamini kuwa litawasaidia katika kuwainua na kuwaongezea ufanisi zaidi na watajikuta wakizidi kulipenda somo la sayansi hadi ngazi ya sekondari na vyuo na baadae kuja kuajiriwa kabisa hasa katika kitengo mbali mbali kama vile madaktari,mainjinia,marubani Nk;

Jumla ya wanafunzi wapatao tisini kutoka shule mbalimbali zilizojitgokeza katika ushiriki huo walifika na kupewa mafunzo hayo ya kisanyansi kwa vitendo bure kabisaa pasipo garama zozote na jambo ambalo limeonekana kuleta mafanikio makubwa kwa wanafunzi wengi kwani nje ya hapo ni kuwa hukutana na kubadilishana mawazo pamoja na kujiona kuwa wapo sehemu sahihi hasa kwa kipaji chao cha kupenda maswala ya kisayansi zaidi


Hata hivyo jamii imeaswa pia katika kuhakikisha inawarusu zaidi wanafunzi kwa ajili ya kujitolea kwa kuwapeleka pale wanaposikia mafunzo kama hayo kwani wapo wazazi wengine ambao hukosa uelewa kuwa mwanafunzi anapopewa mafunzo bora ndio humsaidia katika kupanua na kumuinua katika kipaji chake ndio maana asilimia kubwa ya wanafunzi wamekuwa hawayapendi masomo yao ya kisayansi ushauri huo umetolewa na mzazi wa mawanfunzi Jakline Lekwisa aliemleta mtoto wake ili apate mafunzo hayo pamoja na kujifnza na wenzake.

No comments