TBL Group yaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kuwapatia mafunzo wanafunzi
Mwambawahabari
Wafanyakazi wa TBL Group wakitambulishwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Oysterbay
Afisa wa Masuala Endelevu ,Irene Mutiganzi akiongea na wanafunzi
Afisa Mawasiliano ,Abigail Mutaboyerwa,akisisitiza jambo kwa wanafunzi
Wanafunzi wakimsikiza kwa makini Afisa Mawasiliano kutoka TBL Group,Amanda Walter
Wanafunzi
wa darasa la sita wa shule ya Oysterbay wakiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group,baada ya mafunzo ya kuchambua
changamoto za maisha wakati wa maadhimisho ya siku ya motto wa Afrika
Wanafunzi
wa darasa la sita wa shule ya Oysterbay wakiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group,baada ya mafunzo ya kuchambua
changamoto za maisha wakati wa maadhimisho ya siku ya motto wa Afrika
………………………………………………………………………………
-Pia yaandaa shindano la wanafunzi kuandika insha
Katika
maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwishoni mwa mwiki baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group walijitoa kufundisha wanafunzi wa
shule ya msingi ya Oysterbay iliyopo jijini Dar es Salaam.
Akiongelea
maadhimisho hayo,Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga,alisema
kuwa siku hii ni muhimu kwa kampuni kwa kuwa kupitia sera yake ya
‘Kujenga Dunia Maridhawa’ imelenga kuhakikisha inashiriki
ipasavyo kuhakikisha inachangia kukabiliana na changamoto za kijamii
kwenye maeneo inayofanyia biashara lengo kubwa likiwa ni kuifanya dunia
iwe sehemu bora ya kuishi.
“Sera yetu ya Kujenga Dunia Maridhawa hailengi katika suala la mazigira na maji pekee bali pia kujenga jamii imara na ndio maana tunalipa suala la elimu kipaumbelee kikubwa na leo tumetembelea
shule ya msingi Oysterbay, moja ya shule iliyopo maeneo yetu ya
biashara kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi elimu ya kuwajengea uwezo wa
kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye safari yao ya kielimu na
kutimiza malengo na ndoto zao”.Alisema Tenga.
Alisema baadhi ya maofisa wa TBL Group walipata fursa ya kuongea na wanafunzi wa darasa la sita wa shule hiyo na kuwapatia mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto za
maisha na umuhimu za kuzingatia masomo yao ili waweze kutimiza ndoto
zao za baadaye katika maisha yao ya baadaye wakiwa ni watoto wa
kiafrika.
Tenga alisema mbali na kuwapatia mafunzo kampuni imezindua shindano la wiki moja la kuandika insha ya maneno 300 kwa wanafunzi hao
kuhusiana na changamoto zilizopo katika safari yao ya kielimu na jinsi
ya kuzikabili ambapo wanafunzi watatu wataoshinda watapata zawadi kutoka
TBL .
Alisema
mpango huu wa kukutana na wanafunzi na kuwapatia mafunzo ya kuwajengea
uwezo ni mpango endelevu ambao utaendelea kutekelezwa na wafanyakazi wa
kampuni wenye taaluma mbalimbali katika maeneo yote ambako inaendeshea biashara zake nchini pote.
Siku
ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la
kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya
hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na
jumuiya ya umoja wa Afrika. Elimu kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa
nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Afrika.
Post a Comment