Ads

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KISHAPU

unnamed
Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza na wananchi katika maadhimisho hayo kwenye viwanja vya shule ya msingi Idukilo.
1
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akifurahia jambo na kumpa zawadi mtoto aliyeigiza kama askari katika maadhimisho 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akifurahia jambo na kumpa zawadi mtoto aliyeigiza kama askari katika maadhimisho
3
Ofisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akizungumza neon katika maadhimisho hayo.
4
Sehemu ya watoto wakifuatilia maadhimisho hayo.
5
Diwani wa kata ya Idukilo palikofanyika maadhimisho hayo, Sara Michael akizungumza.
7
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza.
Watoto wa shule wakiigiza kikao cha Bunge namna kinavyofanyika.
9
8
Watoto wa shule wakiigiza kikao cha Bunge namna kinavyofanyika.
10
Sehemu ya watoto wakifuatilia maadhimisho hayo.
11
Kwaya ya watoto wa shule ikiimba wimbo maalumu mble ya wageni wakati wa maadhimisho.
12
Watoto wakionesha umahiri wao wa kuimba wimbo wa kufoka foka ‘Rap’ wenye ujumbe mahsusi.
13
Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akimpongeza na kumkabidhi zawadi mmoja wa watoto waliofanya vizuri katika mitihani yake.
……………………
Na Robert Hokororo
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Shadrack Kangese leo ameongoza wananchi wilayani humo kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kata ya Idukilo, Kangese alisema wazazi wana wajibu wa kuhakikisha wanatengeneza mazingira ya ulinzi kwa watoto wao badala ya kutegemea Serikali pekee.
Alisema wazazi wanapaswa kubeba jukumu la hakikisha watoto hawafanyiwi vitendo vya unyanyasaji na kuwa wanapaswa kutoa huduma muhimu kwao ili waweze kuwa na maendeleo.
Alisema wazazi wanaposhindwa kuwalinda watoto wao matokeo yake hupata matatizo mbalimbali yakiwemo mimba za utotoni hivyo hushindwa hukatiza masomo yao.
Aidha katibu tawala huyo wa wilaya hiyo alikemea tabia ya baadhi ya wazazi wasio waaminifu ambao huwa kikwazo kwa krsi za ukatili dhidi ya watoto zikiwemo za ubakaji na husa.
Aliwataka kutoa ushahidi kwenye vyombo vya usalama pindi watoto wao wanapotendewa ukatili badala ya kukaa kimya kwa maelewano na wanaowafanyia vitendo hivyo.
“Kila siku watoto wetu wanatendewa vitendo vya ukatili vikwemo ubakaji, utekwaji na hivyo hupunguza muda wa kuishi shule zinawajibika kutengeneza mazingira mazuri ya waoto ili wasipopatwe na matatizo haya,” alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga aliwataka wazazi wote kuhakikisha watoto wao wanahudhuria shuleni.  
Magoiga alisema kuwa kama watoto hawaendi shuleni kwa mujibu wa utaratibu haki ya kupata elimu waliyonayo haitakuwa na maana kwani wanakuwa wanakosa masomo.
Alisisitiza kuwa vipaumbele vyake ni vitatu ikiwemo elimu na kuwa katika moja ya huduma ambazo halmashauri inatekeleza kwa wananchi ni elimu kwa watoto wote.
Mkurugenzi mtendaji huyo aliwataka watoto wa kike wasidanganywe bali watumie nafasi waliyo nayo kusoma kwa bidii na kufaulu ili kufikia malengo yao.
Kaulimbi kwa Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka huu ni Maendeleo endelevu 2030: Imarisha ulinzi na haki sawa kwa watoto
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani na maadhimisho haya hufanywa kila Juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na Umoja wa Afrika (EU).

No comments