MTANDAO WA TOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI (TECMN ) WAITAKA SERIKALI NA WADAU MBALIMBALI KUSHIRIKI KIKAMILIFU MAPAMBANO YA NDOA ZA UTOTONI
Na Mtumwa Ally
Mwambawahabari
MTANDAO wa kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN) umeiomba Serikali ,Wabunge pamoja na wadau mbali mbali kushiriki kikamilifu katika kupambana na changamoto zinazopelekea mimba za utotoni ili kulinda haki ya mtoto katika kupata elim bora.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Mkurugenzi wa Mtandao huo,Valeni Msoke alisema hatua hiyo ya kuwashirikisha wadau mbali mbali ni kutokana na kitendo kilichofanywa na baadhi ya wabunge kuunga mkono hoja ya kukatishwa mtoto masomo baada ya kupata ujauzito akiwa shuleni.
Alisema kuwa, sababu zilizotolewa na wabunge wao hazina mashiko yoyote kwani zimejikita zaidi katika maslah yao ya kisiasa ,kwani hazikuzingatia ustawi wa mtoto wa kike na mustakbali wa maisha yake hasa ukizingatia hukumu yenyew inayotolewa anaetakiwa kuacha shule ni msichana tu lakini mvulana yeye anaendelea.
"Sitaki niseme wabunge walioshabikia suala hili hawajui viini vya matatizo yaliopo katika jamii ,lakini ikumbukwe Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mikataba ya kimataifa juu ya kulinda haki ya mtoto na kupata elimu bila kubaguliwa kwa kitu vhochote"alisema Valeni.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa CDF ,Koshuma Mtengo alisema kuwa,utafiti wa kidemografia na Tanzania uliofanywa 2016/17 unaonesha kuwepo kwa ongezeko la mimba za utotoni katika maeneo mengi hususani Vijijini ambapo mkoa wa Katavi ukiwa unaongoza kea asilimia 45.
"Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 32 ya wasichana waliopo vijijini wameathirika na mimba za utotoni ambapo mjini ikiwa ni asilimia 19 tu huku ikiwa zaidi ya asilimia 27 ya wasichana chini ya umri 15-19 wamepata ujauzito kwa mwaka 2015/16 ikilinganishwa na 2010 ilikua asilimia 23"alisema Koshuma.
Aliongeza kuwa,utafiti uliofanywa mwaka 2016 kuhusu vichocheo na madhara ya ndoa za utotoni imebaika kuwa wasichana wengi hawana uwelewa kuhusu elimu ya afya ya uzazi jambo ambalo linapelekea kuongezeka tatizo hili siku hadi siku.
Post a Comment