MD KAYOMBO AMTAKA AFISA MAPATO WA MANISPAA YA UBUNGO KUJITATHIMINI KUTOKANA NA UPOTEVU WA MAPATO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na moja ya wahudumu wa Choo Cha Kituo Cha Mabasi Simi 2000 Mara baada ya ziara ya kushitukiza kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua maeneo mbalimbali ya ukusanyaji Kodi Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimtaza muhudumu wa kituo Cha Mabasi Sinza Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua maeneo mbalimbali ya ukusanyaji Kodi Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua fedha chakavu iliyotolewa na mteja Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na Watumishi wa Manispaa ya Ubungo wanaohudu katika kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato.
Na Mwandishi Wetu, Dar as salaam
Afisa Mapato wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg Fulgence Rweyagaza ametakiwa kujitathmini Kama anafaa kuendelea na majukumu yake ama vinginevyo kutokana na kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya Manispaa katika Kituo Cha Mabasi Simu 2000 kilichopo Kata ya Sinza.
Agizo Hilo limetolewa Jana June 23, 2017 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Mara baada ya ziara ya kushitukiza katika kituo Cha Mabasi Sinza na kujionea Hali ya ukusanyaji mapato isivyo na weledi.
MD Kayombo amebaini kutotolewa risiti ipasavyo ambapo Jambo Hilo limetajwa kuwa ni moja ya sababu ya kupatikana mapato kiduchu ukilinganisha na huduma zinazotolewa Kwa wananchi.
Akiwa kituoni hapo MD Kayombo aliamua kutumia zaidi ya masaa matano kusimama mwenyewe dirishani kukusanya fedha za watu waliokuwa wanapatiwa huduma ya Choo ambapo kwa muda wote huo amebaini uwepo wa fedha nyingi ambazo zilikuwa zinapotea.
Kituo Cha mabasi cha Simu 2000 kina maeneo matatu ya ukusanyaji mapato ambapo ni Choo, Soko pamoja na Daladala.
Katika hatua nyingine MD Kayombo amewafuta kazi watumishi wawili wa kujitolea ambao wamekosa sifa ya kuendelea kuwa wasaidizi katika kazi za Kituo hicho.
Post a Comment