DC MJEMA AWAONGOZA WAKAZI WA JIJI LA DAR SIKU MAZINGIRA
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akimkabidhi kombe Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Osterbay Zefrin Lubuva kuwa mshindi wa Mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani,yaliyofanyika viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akikabidhi cheti kwa Mwandishi wa ITV , Benjamini Mzinga kuwa mmoja wa wadau makini katika utunzaji wa Mazingira
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza katika mkutano wa kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja wa Dar es Salaam.
Na John LuhendeLeo ni siku ya Mazingira Duniani ambapo mkoa wa Dar es salaam maadhimisho hayo yamefanyika katika Wilaya ya Ilala huku kitaifa yakifanyika Butiama mkoani Mara ili kumuenzi Mwana Mazingira wa wakati huo Hayati Mwalimu JK Nyerere.
Akihutubia katika maazimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema amesema Mkoa wa Dar es salaam, unakabiliwa na athari za mabadiliko ya Tabia ya nchi kama ilivyo katika maeneo mengine ya nchi hivyo amewataka watendaji wa mamlaka za Mazingira kutumia kikamilifu sheria zilizopo ili kuthibiti watu wanao chafua Mazingira.
Aidha amesema katika wiki hii ya maadhimisho mkoa wa Dar es salaam umepanda jumla ya miti 10,747 katika maeneo ya wazi , mabondeni ,mashuleni na pembezoni mwa Barabara na pia usafi ume fanyika katika maeneo ya mifereji ,Masoko na fukwe za Bahari na ukaguzi wa vifaa vya makampuni ya usafi pia umefanyika.
Hata hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kuifanya nchi kuwa nchi ya Viwanda kuongeza mapambano dhidi ya dawa za kulevya ,kuhimiza usafi wa Mazingira.
Post a Comment