SBL YAZINDUA BIA MPYA IITWAYO SERENGETI PREMIUM LITE
Mwambawahabari
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara yake, Leah Kihimbi (kulia) ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bia mpya aina ya Lite akitosti glasi na Mkurugenzi
wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta (kushoto) na mjumbe wa bodi ya
SBL, Chris Gachuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa bia hiyo iliyofanyika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Crew nzima ya Kampuni ya PR ya Concept ikiwa katika uzinduzi huo.
Maofisa kutoka SBL wakijadiliana jambo.
Wakati wa utambulisho. Kushoto ni mbunifu wa bia hiyo.
Wasanii wakitoa burudani katika uzinduzi huo.
Mjumbe wa Bodi Chris Gachuma akizungumza katika uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduz huo.
Ni furaha tupu katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza.
Muonekano ya bia hiyo katika chupa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha (wa pili kushoto), akitosti glasi na wanahabari katika uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), mojawapo ya kampuni kubwa
zinazozalisha bia hapa nchini, imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa
ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager iliyoko sokoni kwa
miaka 20 iliyopita.
“Bia ya Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa namna ya kipekee kwa kutumia utaalamu wakisasa.
Ina ladha
kamili inayoburudisha zaidi ya bia za aina ya lite ambazo kwa sasa
huuzwa rejareja sokoni”, alisema Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL,
Kalpesh Mehta, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa kwa Sh.1,500 kwa chupa na
kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuia ya wanywaji wake
ambaokwakipindikirefuwamekuwawakitafuta biahalisiyakitanzania.
“Pamoja
na kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa bia ya
Serengeti Premium Lite, nisemekuwani bia halisi ya kitanzania yenye
kiburudisho na ladha nyepesi.
Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa mudamrefu.
Tunaami
ni kuwa bia hii ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na
kutengenezwa na wazalishajibia (bremasters) wakitanzania kwa watanzania,
itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapokuwa wakifurahia
urithi wetu waaina hii ya bia ”, alisema Mehta.
Aliongeza
kuwa, “Bia ya Serengeti Premium Lite inaubora uleule wa kimataifa sawa
na biamama ya Serengeti Premium Lager ambayoimepokea zaidi ya medali 10
za ubora wakitaifa na kimataifa.”
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na
Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe, aliisifia kampuniya SBL kwa kuwa
inaongoza kwa ubunifu katika sekta ya uzalishaji wapombe nchini, na
vilevile akaahidi kuwa serikali itaendelea kutoa msaada kwa sekta ya
biashara hapa nchini.
Dk.Mwakyembe
ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara
yake, Leah Kihimbi, alisema SBL imekuwa ikishiriki kikamilifu katika
maendeleo ya uchumi wa Tanzania akitaja mafanikio mbalimbali za program
zake za kuisaidijamii.
“Programu
za jamii zinazoendeshwa na SBL katika sekta ya elimu, kilimo na
ujasiriamali zimewezesha vijiji vingi hapa nchini kupata maji safi,
watoto kupata elimu ya juu na mamia ya wakulima kupata masoko kwa ajili
ya kuuza mazao yao ambapo SBL hununua mazao yao kama malighafi
inayotumika kuzalishiabia”, alisema Makamba.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka wizara yake, Leah Kihimbi (kulia) ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bia mpya aina ya Lite akitosti glasi na Mkurugenzi
wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta (kushoto) na mjumbe wa bodi ya
SBL, Chris Gachuma wakati wa hafla ya uzinduzi wa bia hiyo iliyofanyika
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Post a Comment