Watanzania tuone fahari kujivunia muungano wetu:Dkt Salim Ahmed Salim
Na Judith Mhina - MAELEZO
Waziri Mkuu mstaafu wa Awamu ya Kwanza Dkt Salim Ahmed Salim amesema ili muungano
wa Tanganyika na Zanzibar uweze kudumu na kuimarika hatuna budi kuelezea
mafanikio yalitopatikana na pia kutafuta ufumbuzi wa kero chache zilizopo.
Dkt,
Salim Ahmed Salim amesema hayo leo jijini Dar Es salaam wakati wa mahojiano na
Idara ya Habari – MAELEZO kuhusiana namaadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika hizi karibuni.
Warizi
huyo msataafu amekiri kwamba Watanzania wana haki ya kujivunia muungano huu
ambao ni wa asili kutokana na mahusiano yetu ya kindugu hata kabla ya Muungano.
“Mahusiano ya kindugu baina ya Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar ni ya
miaka mingi ambapo watu wake wamekuwa wakitembeleana na kuoana. Aidha,
mahusiano hayo yameonekana katika masualoa ya kijamii kama vile lugha, dini n.k.
Dkt
Salim ameeleza kwamba, walichokifanya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere na Hayati Shekh Abeid Amani Karume ni kuweka uwazi juu ya
mahusiano ya watu wa Tanganyika na Zanzibar duniani hususan kwa wale ambao
hawajui asili ya watu wa pande hizo mbili.
“ Jambo
hili la Muungano kudumu miaka 53 linashangaza watu wengi duniani, hasa kwa
dhana kwamba nchi za kiafrika zina matatizo, na sio rahisi kuelewana. Jambo
kubwa linalofanikisha kudumu kwa Muungano wetu ni umoja, upendo na
mshikamano. Tumekuwa tukuweka wazi mafanikio na pale penye changamoto hukaa
pamoja na kuzungumza ili kuyapatia ufumbuzi.”
Akizungumzia
suala la vijana kushika madaraka Serikalini, Dkt Salim amesema “Hii si jambo
geni kwani mimi ndiye kijana wa kwanza ambaye niliaminika nikiwa mdogo
sana miaka 22 na kuteuliwa kuwa Balozi nchini Misri. Kazi hii haikuwa ndogo
lakini niliifanya kazi kwa kujiamini na kwa uadilifu mkubwa huku nikipata
maelekezo kutoka kwa viongozi wangu wakuu (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar).
Hivyo
napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa Watanzania wenzangu hususan vijana
wanaoaminiwa na Taifa katika umri mdogo kushika uongozi wakubali nafasi hizo
kwa kuwa bado wana nguvu ya kuweza kulitumikia Taifa letu. Lakini wasisahau
kuwasikiliza viongozi waliowapa nafasi hizo, na ushauri wa wazee ni muhimu
sana. Aidha, wajue kuwa nafasi za uongozi wanazomepewa kuwawakilisha Watanzania
zilete maendeleo ya kweli.
Akielezea
mustakabali wa maendeleo ya nchi, Dkt Salim alitolea mfano wa vijana wa Afrika
ya Kusini ambapo hivi katibu alikwenda kushiki moja ya mikutano viongozi wa
nchi za Afrika. hivi Amesema, vijana wa Afrika ya Kusini hawataki kusikia
lolote zaidi ya mambo yanayowahusu wao na maisha yao. Hawajui kama kuna watu
wamepigania uhuru na hatimaye ukombozi wa nchi yao. Wao hilo si
kipaumbele kwao, wanachotaka ni maendeleo ambayo yatagusa maisha yao.
“Hivyo
ni vema Serikali zetu zilivyoamua kuelekeza nguvu katika viwanda vidogo vya
kati na vikubwa, kwa sababu malighafi tunazo za kutosha ila tulikosa mbinu za
kuongeza thamani ya malighafi zetu. “Nataka nikuhakikishie tuko kwenye njia
sahihi ili kuwafanya vijana walio wengi washiriki katika kulijenga Taifa na
kupata ajira ambazo zitawafanya waishi kwa furaha na matumaini,” Asema Dkt
Salim.
Akijibu
swali, kuhusiana na lipi la kujivunia kutokana na Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar Dkt Salim amesema : “ Umoja wetu ndio uliotufikisha miaka 53,
tusingekuwa wamoja tungegawanyika na Muungano ungekuwa mashakani. Angalia
idadi kubwa ya Watanzania sasa ni wale waliozaliwa baada ya Muungano ambao
hawajui lolote kuhusu Muungano.
Tuna
Jukumu kubwa la kuendeleza elimu ya historia kwa vizazi vya sasa na vijavyo
waelewe na kudhamini kazi zilizofanywa na waasisi wetu wa Muungano Mwalimu
Nyerere na Shekh Karume. Mfano mzuri ni Taifa la China ambalo vijana wengi
hawakuwahi kumuona Mao SeThung, lakini wanamjua kutokana na historia
wanayoelezwa na matunda yake ambayo wanayaona.
Pili,
Watanzania tusibaguane kama alivyosema Mwalimu Nyerere kwamba dhambi ya ubaguzi
haiwezi kuishia hapo unapombagua mtu, itaendelea kwa mwingine na mwingine na
mwisho Taifa litagawanyika.
Aidha,
Dkt Salim amesema kwamba Taasisi ya Mwalimu Nyerere itaendelea kutoa elimu ya
umuhimu wa muungano ambao ni tunda la umoja na mshikamano barani Afrika,
hususani Tanzania ambao wanahitaji kuwa na elimu ya uraia.
Mwisho
alimalizia kwa kutoa wito kwa Watanzania kuuenzi na kudumisha muungano wetu
ulioanzishwa na Waasisi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Shekh Abeid
Amani Karume.
Post a Comment