VIJANA DAR ES SALAAM WAANZISHA KLABU ZA MABADILIKO KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI
Mwezeshaji
wa Kisheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mariam Rashid
(kulia), akitoa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa vijana
wafanyabiashara katika Soko la Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam
kabla ya kufungua klabu za mabadiliko za kupinga ukatili huo katika soko
hilo mwishoni mwa wiki.
Mwezeshaji
wa kisheri Juliana Charles akichukua jina na maelezo kwa mfanyabiashara
wa soko hilo aliyekubali kuwa mwana mabadiliko wa kupinga vitendo vya
ukatili wa kijinsia.
Mwezeshaji
wa kisheria Charles Beatus (katikati), akiwa na vijana wa klabu ya
wauza nguo za mitumba ya kike katika soko la Ilala Mchikichini
wakibandika bango la mabadiliko.
Vijana wa mabadiliko wa Soko la Ilala Mchikichini wakiwa
kataika picha ya pamoja.
Mwanasheria
wa EfG, Muna Abdallah akichukua maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Klabu
ya Mabadiliko ya wauza nguo za kike katika soko la Ilala Mchikichini,
Adam Mohamed (kushoto)
wanamabadiliko wakionesha vipeperushi vya kampeni ya Tunaweza baada ya kufungua klabu hizo.
Mwezeshaji wa kisheria Zainabu Namajoji akichukua maelezo
kwa wanamabadiliko.
Vijana
wafanyabiashara katika Soko la Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam
wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa kisheria wa Shirika la
Equality for Growth (EfG), wenye fulana za njano, baada ya kufungua
klabu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo
mwishoni mwa wiki.
Maelezo yakichukuliwa.
Na Dotto Mwaibale
VIJANA
wafanyabiashara katika masoko ya Temeke Sterio na Ilala Mchikichini
jijini Dar es Salaam wameanzisha klabu za mabadiliko zitakazo saidia
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia masokoni kupitia kampeni ya
miezi miwili ya Tunaweza inayofanywa na Shirika la Equality for Growth
(EfG).
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wafanyabiashara hao wamesema
kwamba wameamua kuanzisha klabu hizo za mabadiliko na kushiriki kampeni
hiyo baada ya kuhamasishwa na wasaidizi wa kisheria wa Shirika la
Equality for Growth (EfG) kuhusu kutokomeza vitendo vyote vya ukatili wa
kijinsia katika maeneo yao ya biashara.
“Kampeni
hii tumeikubali na ndio maana baada ya kuhamasishwa na EfG tumeamua
kufungua klabu za wanamabadiliko kwani tumeona inatujengea mazingira
mazuri ya kufanya biashara zetu katika eneo ambalo halina vitendo vya
ukatili wa kijinsia” alisema Adam Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa klabu
ya mabadiliko eno la wauza nguo za mitumba ya kike Soko la Ilala
Mchikichini.
Alisema
kwa muda mrefu katika soko hilo kulikuwa na kukithiri kwa vitendo hivyo
lakini kupitia kampeni hizo imesaidia kuvipunguza na kuwa baada ya
kupata mafunzo hayo kutoka EfG wamekuwa wakiifanya kampeni hiyo hata nje
ya masoko ili jamii ijue umuhimu wa kuachana na vitendo vyote vya
ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti
wa klabu ya wauza viatu na raba katika Soko la Ilala Mchikichini,
Philip Chuwa alisema klabu zilizoanzishwa zitasaidia kukabiliana na
vitendo hivyo kwa kuwa wanachama wake ni wafanyabiashara wenyewe hivyo
itakuwa rahisi kumbaini mtuhumiwa na kumchukulia hatua.
Akizungumzia
kampeni hiyo ya Tunaweza Mwanasheria na Mratibu kutoka Shirika la EfG,
Mussa Mlawa alisema kampeni hiyo inaendeshwa na Kituo cha Msaada wa
Sheria kwa Wanawake Tanzania (WLAC) lakini katika masoko inafanywa na
EfG.
Alisema lengo la kampeni hiyo ni kusukuma mabadiliko ya kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia masokoni na katika jamii.
Alisema
kampeni hiyo kwa Dar es Salaam inafanyika katika masoko matano ya Ilala
Boma, Mchikichini, Temeke Sterio, Buguruni na Ferry.
Post a Comment