MRADI WA KUHAMASISHA WANAWAKE NA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA UWAKILISHI WA KISIASA (WRPRE PROJECT) WAZINDULIWA
Kamishna wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa
Mradi wa Woman And Youth Political Participation Enhanced In 2019 Aand
2020 General Election In Tanzania uliofanyika kwenye hoteli ya New
Africa jijini Dar es salaam leo na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka
,Serikalini. Vyama vya siasa, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na
Asasi za Kiraia.
Mradi huo utakaotekelezwa na
Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA na TYC na WE Effect huku
ukifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa kiasi cha sh ilingi Bilioni 1.4na
utatekelezwa kwa miaka mitatu.
Lengo la Mradi huo ni Kuongeza
Ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uwakilishi wa kisiasa katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2019-2020 katika ngazi zote za uongozi kuanzia
ngazi za vijiji hadi taifa, Mradi huu pia unalenga kuangalia vizuizi
vinavyokwamisha wanawake na vijana kushiriki kwenye mchakato wa kugombea
uongozi wa kisiasa na kuangalia ni jinsi gani vizuizi hivyo vinaweza
kutatuliwa.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya
Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Roeland Van De Geer akitoa
ujumbe wake kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa mradi huo, Jumuiya ya
Ulaya ndiyo iliyofadhili mradi huo .
Mwenyekiti wa Chama cha
Wanasheria wanawake TAWLA B. Athanasia Soka akizungumza wakati wa
uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar
es salaam.
Mama Anna Mngwira aliyekuwa
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 na
mwanachama wa Chama cha wanasheria wanawake akifuatilia kwa makini
uzinduzi wa mradi huo
Baadhi ya waalikwa katika
uzinduzi huo wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa
mashirika na taasisi za serikali.
Mkurugenzi wa Chama cha
Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile akitambulisha wageni
mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akikaribishwa na Mwenyekiti wa Chama cha
Wanasheria wanawake TAWLA B. Athanasia Soka wakati alipowasili kwenye
hoteli ya New Africa kwa ajili ya uzinduzi wa mradi huo.
Baadhi ya maofisa kutoka TAWLA wakisimamia uasili na kuwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Mkurugenzi wa Chama cha
Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile pamoja na wageni waalikwa
wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
Afisa kutoka Makao Mkuu ya CCM Ofisi Ndogo ya Lumumba Bw. Suleiman Mwenda pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akiwa katika
picha ya pamoja na wageni waalikwa katika mara baada ya uzinduzi huo.
Post a Comment