Ads

Marekani: Hatuna Muda wa Ziada wa Kuvumilia Vitisho vya Korea Kaskazini

Mshauri wa Rais Donald Trump wa masuala ya usalama, Herbert Raymond McMaster amesema kuwa Marekani na China zinaelekea kupoteza uvumilivu dhidi ya Korea Kaskazini inayoendelea na vitisho vya silaha za Nyuklia.

McMaster amesema makubaliano yanayojitokeza dhidi ya tabia ya vitisho vya Korea Kaskazini kwa sasa yanaijumuisha China. 

Amesema kuwa kuna makubaliano ya kimataifa, ikiwemo China kuhakikisha tabia hii haiendelei, kwani kumekuwa na majaribio ya makombora ya hivi karibuni yanayoonyesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini hali ambayo hawataivumilia zaidi.

Amesema kuwa Rais Trump ameweka wazi kuwa Marekani na washirika wake hawatokubali kuona utawala wa vitisho dhidi ya silaha za nyuklia.

Korea Kaskazini imefanya jaribio la uzinduzi wa makombora ya masafa ya mbali, hata hivyo lilikwama, ambapo Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amefika Korea Kusini saa chache baada ya jaribio hilo.

Akizungumza katika kambi ya jeshi, Pence amesema anawahakikishia kuwa chini ya uongozi wa Rais Trump ushirika wa  Marekani  Korea Kusini haujawahi kuwa na nguvu lakini kwa msaada wa jeshi hilo na Mungu uhuru utaendelea kuimarika katika rasi ya Korea bila vitisho vyovyote

No comments