Breaking News: Watu 2 wamefukiwa na Kifusi katika machimbo ya golani eneo la Pugu
Friday, April 07, 2017
Mwambawahabari
Kwamujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mama Sophia Mjema Watu hao wamefukiwa na Kifusi katika machimbo ya kokoto Jana majira ya Saa Nanne Mchana, Lakini mpaka sasa hawajafanikiwa kuwaokoa kulingana na changamoto ya Mvua zinazoendelea kunyesha lakini pia ubovu wa miundombinu njia za kupitishia Mitambo ya uokoaji.
Aidha amewataja walio naswa na kifusi kuwa ni Rashid , Shabani Amosi katika Boni na Rashidi
Kamanda wa Polisi wa IlalaSalum Hamduni akizungumza na waandishi wa habari eneo la tuko hapo akijibu swali la Mwandishi wa mwambawahabari blog aliye upande wa kushoto John Luhende ambaye amepiga kambi kufuatilia tuko hilo..
Kwamujibu wa kamanda huyo machimbo hayo yalikuwa yamepigwa marufuku na serikali miaka miwili iliyopita lakini wananchi hao walikaidi amri hiyo na kuendelea kufanya kazi za uchimbaji wa kokoto katika eneo hilo .
Hata hivyo Mwamba wa habari imezungumza na mmoja wa mashuhuda wa tuko hilo ....Mohamedi ismail..amesema yeye alikuwa na na ndugu yake naye amenaswa na kifusi na walifanikiwa kuokoa mwili wake na maiti yake ameimehifadhiwa katika hospital ya Taifa Muhimbili. Na ameshauri wananchi hao kuacha kufanya kazi hizo kwa kuwa eneo hilo ni hatarishi.
Post a Comment