WILAYA YA DODOMA YAZINDUA KAMPENI YA MAGAUNI MANNE YENYE LENGO LA KUPINGA MIMBA ZA UTOTONI
Mwambawahabari
Jumla ya shule za Sekondari 9 ambazo ni baadhi ya shule zilizopo katika
Manispaa ya Dodoma leo Machi 10 zimeweza kushiriki katika kampeni ya
Kihistoria ya kupinga vita mimba za Utotoni hasa kwa wanafunzi wa Shule
za Msingi na Sekondari katika kampeni inayoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa
Wilaya hiyo ya Dodoma, Bi. Christina Mndeme inayoitwa ‘Magauni Manne.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Dodoma, Bi. Idaya Maenda amebainisha kuwa, suala la mimba za utotoni ni
kubwa kwa Manispaa hiyo hivyo anampongeza Mkuu wa Wilaya ya kuanzisha
kampeni hiyo ya magauni manne kwani itasaidia kuwajenga wanafunzi
kupenda masomo na kukataa vishawishi.
“Tunaomba hatua za haraka zichukuliwe.
Pia ushirikiano baina ya wazazi na Serikali kwani Wazazi wengi wamekuwa
wakikwamisha zoezi la kupambana na mimba za utotoni kwa kuwakataza
watoto wanaopata mimba kuwataja ama kuwafichua wanaume wanaowapa mimba
hizo.
Hali ya mimba kwa Manispaa inatisha
kwani Shule za Msingi jumla ya wanafunzi 6, wameweza kupata ujauzito
kwa kuanzia 2016 mpaka sasa. Ila kwa takwimu za shule za Sekondari ,
jumla ya wanafunzi 54 wameweza kupata mimba kwa mwaka 2016. Kwa
takwiamu za mwaka huu 2017. Kwa kipindi cha Januari hadi mwezi huu wa
Machi, zaidi ya wanafunzi 18, wamepata ujauzito na kufanya kwa kipindi
chote cha 2016-2017, kuwa na jumla ya wanafunzi 74, Hali hii inatisha
sana hivyo tunaamini kampeni ya magauni manne itasaidia kuwajenga watoto
kukataa vitendo vya kishawishi.” Amesema Bi Idaya Maeda.
Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi
kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bi Christina Mndeme amebainisha
kuwa, ili kuweza kupinga vita ya mimba za utotoni amewataka wadau kwa
pamoja kumuunga mkono katika sualla hilo huku akiimiza ushirikiano kwa
wazazi na walimu katika kumfuatilia mtoto wao wakati wote wa masomo.
“Tunawaomba sana. Wazazi kuwa na wakati
wa kuwa karibu na watoto wenu. Kujua wanasoma nini shuleni na pia
kujua tabia zao mara kwa mara. Pia nitoe wito tu, watoto wangu, kataeni
kushawishiwa na waendesha bodaboda. Kataeni ofa zao kwani ndizo
zinawasababishia vishawishi na kupata ujauzito.
Tutakae mbaini akiwarubuni wanafunzi
hasa vijana wa bodaboda na nyie wauza Chipsi huko mitaani basia hatua
kali zitachukuliwa. Tuwaache watoto wetu wasome na watimize malengo yao
katika mustakabali huu wa magauni manne” alieleza Mkuu wa Wilaya huyo
Bi. Mndeme.
Mkuu wa Wilaya amebainisha kuwa, suala
la mimba za utotoni ni kubwa hivyo ameamua kuanzisha kampeni hiyo na
anaamini itafanikiwa kwa kiasi kikubwa ni itamjenga mwanafunzi kutimiza
malengo yake, ambapo Magauni manne ikiwa na maana ya gauni la kwanza ni
vazi la shule kwa mwanafunzi huku gani la pili ni Joho la mwanafunzi
wakati wa kuhitimu kiwango chake cha elimu ya juu ambacho Taifa
inakitaka kwa watu wake kuanzia elimu ya chini mpaka ya juu, hivyo hivyo
kwa gauni la tatu ni la Harusi ambalo tayari ameshamaliza elimu yake na
anaweza kuamua kile alichokuwa anakitamani muda mrefu huku gauni la
mwisho ni lile la ujauzito ambalo alikuwa na ndoto nalo kwa muda mrefu.
Aidha, katika tukio hilo pia limeweza
kushuhudiwa na watu mbalimbali akiwemo Mbunge wa Dodoma Mjini Antony
Mavunde, Mbunge wa viti maalum Bi. Felista Bula. Pia walikuwepo Mc
Pilipili, Maimatha Jese na wengine wengi ambao ni wazawa wa Mkoa huo wa
Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Bi. Idaya Maenda akielezea wakati wa mkutano huo
Mwanadada
Maimatha Jese akitoa maelezo mafupi na ya kuwapa moyo wanafunzi wa kike
katika kuzingatia masomo na kuepuka mimba za utotoni.
Mbunge wa viti maalum Dodoma, Bi. Felista Bula akiwaelezea jambo wanafunzi hao wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde akizungumza katika mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bi Christina Mndeme katikati akifuatilia matukio yaliyokuwa yakiedelea
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Bi Christina Mndeme katikati akiwa na wanafunzi
wakionesha alama ya vidole vinne kuashiria kampeni ya magauni manne.
Kulia ni mwendesha shughuli MC Pilipili
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bi Christina Mndeme katikati akiwa na wanafunzi waliovaa mfano wa magauni manne
Post a Comment