Ads

SHULE YA ALMUNTANZIR YANDAA MATEMBEZI YA KUTOA ELIMU KUHUSU WATU WENYE USONJI (AUTISM)


Displaying IMG-20170329-WA0005.jpg

Na John Luhende Mwambawahabari
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi  wenye  Watoto wenye mahitaji maalumu  kutowaficha ndani na kuwa acha bila msaada  watoto wenye matatizo ya  Usonji   na kutambua kuwa  ni zawadi kutoka kwa Mungu  na wanastahili kupatiwa  Elimu sawa na watoto wengine .

Akizungumza na waandishi wa habari kwaniaba ya mkuu wa shule hiyo mwalimu mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Wasichana Almuntazir  (AMSEN)  Bi Joan  Soka    ameitaka jaamii kuto watenga watoto hao kwa kuwa nawao wanahakisawa na watoto wengine na wana haki ya kupatiwa Elimu .

Aidha  Soka  amesema matembezi hayo yata saidia kuhamasisha jamii kuwa na uelewa kuhusu watoto hao wenye matatizo ya usonji uliko ilivyo sasa ambapo wato wengi wenye matatizo jamii haiwajali.

Pamoja na hayo Amesema kuwa tangu kuanzishwa  kwa shule  hiyo mwaka 2013 watoto wengi walio soma  shule hiyo  wamesaidiwa kupata elimu na  ambayo imeweza kuwa saidi a katika maisha yao na baadhi yao wameajiriwa  kufanya kazi katika taasisi na makampuni kufanya kazi mbalimbali kulingana na halizao  na wame weza kujipatia kipato.


Matembezi hayo  yanafanyika kwa mara ya pili  na yatafanyika siku ya  Usonji Duniani (AUTISM DAY)  tarehe 2/  April 2017   saa 2: 30  yata anzia shule ya  Shule ya Wavulana Almuntazir   na kuishia katika Shule ya wasicha  Almuntazil  ,,,,,,Kauli mbiu mwaka huu ni  ‘’ Tuwalinde na Tuwapende,,



No comments