MEYA WAJIJI KUHUDHURIA MKUTANO WA SERIKALI ZA MITAA WA DUNIA AFRICA YA KUSINI
NA Christina Mwagala ,Dar
mwambawahabari
MEYA wa jiji la Dar es Isaya Mwita leo ameondoka nchini kuhuzuria mkutano wa siku tatu wa munganiko wa serikali zamitaa duniani ( ICLEI ) utakaofanyika huko nchini Afrika Kusini hapo kesho.m
Mkutano huo ambao utahusisha mameya wote wa Afrika, utajikita kushugulikia mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuhakikisha matumizi mazuri ya utumiaji wa rasilimali za nchi.
Aidha kupitia mkutano huo ikiwemo kujadili mabadiliko ya tabia ya Nchi, itajikita zaidi hususani kujikinga na majanga ya mafuriko pamoja na kutafuta suluhisho la matatizo ya maji kwenye majiji.
Katika suala la maji ,mkutano huo meya wa jiji atawasilisha mada inayohusiana na kuondokana na tatizo la maji katika jiji la Dar es salaam kupitia vyanzo vya maji ikiwemo Ruvu chini, Kimbiji pamoja na vyanzo vingine.
Aidha kwa upande wa suala zima la mafuriko, Meya Isaya pia atawasilisha mada kuhusiana na mafuriko ambapo katika mkutano huo wote kwa pamoja watajadili pamoja na kujengewa uwezo katika kuendesha majiji yao sambamba na kukabiliana na majanga yaliyopo.
Itakumbukwa kwamba jiji la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji ambayo hukumbana na changamoto ya mafuriko, ambapo kupitia mkutano huo wakazi wa jijini hapa itawasaidia kuondanokana na changamoto hiyo.
Meya wa jiji atarejea nchini Machi 25 mwaka huu.
Post a Comment