WANASHERIA WA KUJITOLEA MKOA WA DAR ES SALAAM WAKABIDHI TAARIFA YA UTENDAJI KWA RC MAKONDA.
Na John Luhende
mwambawahabari
Wanasheria wa kujitolea wa mkoa wa Dar es salaam walio itikia ombi la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe, Paul Makonda kuwataka wanasheria kuwa saidia wananchi wa mkoa huo kuhusu mambo ya kisheria leo wamekabidhi taarifa ya utendaji wa kazi hiyo kwa kipindi cha kuanzia 16/12/2016hadi 24/2/207.
Akiwasilisha taarifa hiyo kiongozi wa wanasheria hao Geogia Kamina amesema wamehudumia wananchi 10217 na jumla ya kesi kesi 701 ziliweza kusikilizwa ikiwemo migoro ya ardhi , kazi , mirathi na ndoa ,pamoja na kushugulikia migogoro sugu ilikaazaidi ya miaka kumi na sasa imekwisha , na kusema kuwa wanaishukuru serika kwa kuanzisha utaratibu huo kisheria .
Aidha Kamina amefafanua kuwa wanasheria hao waligawanyika katika wilaya zote za mkoa huo na walihudumu kwa makundi, wanasheria waliohudumia wilaya ya Kigamboni walihudumia wananchi 29 na kusikiliza kesi 18, Ubungo walisikiliza kesi 37 na kuhudumia wananchi ,806, Temeke walisikiliza kesi 200 nakuhudumia wananchi 20211, Kinondoni walisikiliza kesi 18 na kuhudumia wananchi776 , Ilala walisikiliza kesi 266 na walihudumia wananchi 3279 katika kipindi cha mwezi mmoja.
‘’Moja ya kesi ambayo ilitutia changamoto ni kesi ya mirathi ambayo faili la kesi hiyo lilipotea na shukurumungu tulifuatilia hadi faili hilo lilipatikana kesi hiyo ilidumu muda wa miaka kumi na mama huyo mjane alipatahaki yake’’ alisema mwanasheria Kamina
Ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni wananchi wengi hawana uelewa kuhusu mambo ya kisheria hivyo ndhahiri kuwa wanachi wanauhitaji mkubwa wa msaada wakisheria.
Naye mkuu wa mkoa mko huo mhe. Paul Makonda amewashukuru wanasheria hao na kuwa tia moyo kuwa kwa kazi hiyo kuwa imetia hamasa kwa wanasheria wengine na kuwataka wanasheria wengine kuiga mfano wa wanasheria hao kwa kufanya kazi za kujitolea kuisaidia jamii katika matatizo ya kisheria ametoa rai kwa wana kwa wanasheria wa nkoa huu mwendelee kuwa saidia wanyonge akina mama na wote wasiojiweza katika kupata huduma za kisheria .
‘’Mji huu unawajanja wengi na nchi yetu si wote tulibahatika kwenda shule wajanja hutumia fursa hiyo kuwa kandamiza wengine nawashukuru sana wanasheria wote mlioshiriki katika kazi hii’’ alisema Makonda

Post a Comment