Ads

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ,MAJ.GEN MILANZI AWAONYA WAHITIMU WA MAFUNZO YA JESHI USU KWA WAHIFADHI WA WANYAMAPORI 103

 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza kwenye mkutano uliofanyika jana mjini Morogoro ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) walipokutana na Wahifadhi Wakuu wa Mapori ya Akiba nchini kwa lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la ujangili. 
mwambawahabari
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, amesema hatamvumilia mtumishi  yeyote atayejihusisha na vitendo vya rushwa kuwa ni lazima ataondolewa mara moja  ili asiendelee kuchafua taswira ya Wizara.
Alitoa rai hiyo  jana wakati akifunga mafunzo ya jeshi Usu kwa  wahifadhi wa
wanyamapori  103 kutoka Mamlaka ya Hifadhi  Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori    ( TAWA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA).

Alisema Wizara kwa sasa  inabadili mfumo wa kiraia  na kuendesha kwa  mfumo wa kijeshi hivyo mtumishi yeyote asiyejihusisha na vitendo viovu vya namna yeyote Yule hatasalimika.
Wakati huo huo , Maj. Gen. Gaudence  Milanzi alifungua mafunzo ya ukakamavu kwa  maafisa wanyamapori wa daraja la pili  kutoka TAWA yatakayochukua muda wa wiki tano  lengo likiwa ni kuwandaa watumishi wa taasisi hiyo katika kuboresha mbinu za kupambana na majangili.

 
Akizungumza jana na wahitimu hao kabla ya kufunga  mafunzo hayo katika kituo cha Mafunzo cha Mlele mkoani Katavi ,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi aliwataka  wahifadhihao wakaoneshe kile walichojifunza kwa  kwa kujenga mahusiano mazuri na wanavijiji wanaozunguka hifadhi  nchini baadala ya kujenga uadui.
Aliwasihi wahitimu hao kutumia silaha kwa weledi pale inapobidi hasa inapohitajika
kunusuru maisha ya watu na sio kuua.

Aidha,Milanzi aliwaagiza wakuu na viongozi  wa taasisi  zote zilizo chini ya Wizara  wahakikishe   wanashiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa Wizara inatoka kwenye mfumo wa kiraia na kuelekea kwenye  mfumo wa kijeshi katika utendaji wa shughuli za uhifadhi nchini.
Akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii,
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, David Kanyatta aliwataka wahifadhi waliopewa mafunzo hayo wakajitume kwa kufanya kazi kwa bidii  katika vituo vyao vya kazi ili kuonesha tija kwa taifa katika uhifadhi.


 
 Kabla ya kuwahutubia wahitimu hao, Katibu Mkuu Milanzia alioneshwa mbinu mbalimbali kwa vitendo walizojifunza katika kupambana majangili ambao wamekuwa wakitumiasilaha nzito wakati wakifanya ujangili.
 

No comments