WAKAMATWA KWA KUGUSHI NYARAKA ZA USAJILI WA GAZETI ,BAADA YA MAELEZO KUBAINI
mwambawahabari
Mkurugenzi Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari hawapo (pichani) kuhusu kukamatwa kwa mmiliki wa Kampuni ya FAKUNA ambaye anatuhumiwa kutaka kuitapeli Serikali baada ya kubainika kuwasilisha nyaraka za kughushi ili asajili Gazeti la Lete Mambo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Msajili wa Magazeti Patrick Kipangula na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Lilian Lundo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO aalipokuwa akitoa taarifa juu ya kukamatwa kwa mtuhuhiwa aliyejaribu kughushi nyaraka za Serikali ili asajili Gazeti leo jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa wa kughushi nyaraka za Serikali ili asajili Gazeti ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya FAKUNA Bw. Joseph Sheka akitolewa ndani ya Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO punde baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO kumkabidhi mtuhumiwa huyo mikononi mwa jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua zaidi.
Pichani mtuhumiwa Joseph Sheka akiongozwa na Askari Kanzu kuelekea kwenye gari la Polisi tayari kwa kupelekwa Kituo cha Polisi Kati leo jijini Dar es Salaam. Sheka anatuhumiwa kutaka kuitapeli Serikali kwa kuwasilisha nyaraka za kughushi katika Ofisi za Msaji wa Magazeti ilia pate usajili wa Gazeti la Lete Mambo.
Watuhumiwa wakiwa ndani ya Gari la Polisi mara baada ya kukamatwa na kukabidhiwa kwa jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam.Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati kwa mahojiano zaidi na hatua zingine zitafuatia.
Picha na: Frank Shija
Post a Comment